• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC ARUSHA APONGEZA NA KUZINDUA MADARASA YA MPANGO WA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO 19 ARUSHA DC

Posted on: December 16th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amekabidhiwa na kuzindua vyumba 9 vya madarasa katika shule 5 za sekondari halmashauri ya Arusha, huku akiwapongeza wasimamizi wa mradi huo kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri, kata, viongozi wawakilishi wa wananchi pamoja na wananchi wote kwa ushiriki wao, kwa kukamilisha miradi hiyo kwa viwango na kwa wakati.

Mkuu huyo wa mkoa, ametoa pongezi hizo mara baada ya kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19, ambapo alipokea na kuzindua madarasa 9, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua  miradi hiyo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.

"Ninawapongeza wananchi wote wa halmashauri ya Arusha kwa ushirikiano mliuonesha katika kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa madarasa, madarasa yamejengwa kwa viwango vinavyohitajika na kukamilika kwa wakati, madarasa yanavuti,  hii maomesha dhahiri namna gani mnaunga mkono agenda ya mheshimiwa Rais, mama Samia ya kuboresha huduma za jamii na kuondoa kero kwa wananchi, hongereni sana ofisi ya mkuu wa wilaya, timu ya watalamu halmashauri, waheshimiwa madiwani pamoja na wananchi wote kwa ujumla wenu" amesisitiza Mhe. Mongela

Aidha, mheshimiwa Mongela amewataka wananchi kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kuwa serikali imeleta fedha nyingi katika miradi ya elimu, afya, maji na barabara, serikali inahitaji ushiriki wa wananchi, ushiri ambao utawezesha umiliki wa wananchi wa miradi hiyo baada ya kukamilika.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Mongela, amewaagiza watendaji, wanachi na  wadau wa maendeleo wa halmashauri hiyo, kuweka mkakati wa kukamilisha miradi mingine ya madarasa ambayo imejengwa kwa nguvu za wanachi na haijakamilika katika shule za halmashauri hiyo na kuhakikisha, miradi hiyo inakamilika ili wanafunzi watumie madarasa hayo.

Katika ziara hiyo viongozi wawakilishi wa wananchi, wameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita na juhudu za mhesimiwa Rais, mama Samia Suluhu kwa kuelekeza fedha nyingi, kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za halamshauri ya Arusha, jambo ambalo wamekiri halijawahi kutokae na kuongeza kuwa, fedha hizo za ujenzi wa madarasa zimekuja wakati muafaka kwa kuwa kila mwaka, wananchi hulazimika kuchangishana kujenga madarasa ya kidato cha kwanza kwa mwaka unaofuata.

Diwani wa kata ya Bangata Mhe. Ezra Tomito amesema kuwa licha ya kuwa madarsa hayo yatawanufaisha watoto wao, lakini kwa kiasi kikubwa yamewapunguzia wananchi mzigo wa kuchangishana fedha za ujenzi wa madarasa, zoezi ambalo hufanyika kila mwaka nyakati kama hizo.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amemshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha,  kwa kukuabali kupokea na kuzindua vyumba 9 vya madarasa, kama mfano wa madarasa yote yaliyokamilika katika halmashauri ya Arusha, na kumuhakiksihai kuendelelea kusimamia utekelezaji wa majukumu ya serikali ya kuwatumikia wananchi, pamoja na kuyafanyia kazi maagizo yote  aliyoyatoa ikiwemo kusimamia fedha  zilizoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi katika sekta zote na kuweka mkakati wa kukamilisha miradi viporo ya madarasa katika shule.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, ametembelea jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi milioni 860, miradi 7 ya sekta ya elimu na mradi mmoja wa upanuzi  wa kituo cha Afya Oldonyosmabu unaogharimu shilingi milioni 200.

Ikumbukwe kuwa, halmashauri ya Arusha ilipokea shilingi bilioni 2, fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19,  za ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa, kwa mgawanyo wa madarasa 96 shule za sekondari na madarasa 4 kwa shule mbili za msingi shikizi, madarasa yote yanatakiwa kujamilika ifikapo 31, Desemba, 2021.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.