Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amekabidhiwa na kuzindua vyumba 9 vya madarasa katika shule 5 za sekondari halmashauri ya Arusha, huku akiwapongeza wasimamizi wa mradi huo kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri, kata, viongozi wawakilishi wa wananchi pamoja na wananchi wote kwa ushiriki wao, kwa kukamilisha miradi hiyo kwa viwango na kwa wakati.Mkuu huyo wa mkoa, ametoa pongezi hizo mara baada ya kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19, ambapo alipokea na kuzindua madarasa 9, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi hiyo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru."Ninawapongeza wananchi wote wa halmashauri ya Arusha kwa ushirikiano mliuonesha katika kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa madarasa, madarasa yamejengwa kwa viwango vinavyohitajika na kukamilika kwa wakati, madarasa yanavuti, hii maomesha dhahiri namna gani mnaunga mkono agenda ya mheshimiwa Rais, mama Samia ya kuboresha huduma za jamii na kuondoa kero kwa wananchi, hongereni sana ofisi ya mkuu wa wilaya, timu ya watalamu halmashauri, waheshimiwa madiwani pamoja na wananchi wote kwa ujumla wenu" amesisitiza Mhe. MongelaAidha, mheshimiwa Mongela amewataka wananchi kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kuwa serikali imeleta fedha nyingi katika miradi ya elimu, afya, maji na barabara, serikali inahitaji ushiriki wa wananchi, ushiri ambao utawezesha umiliki wa wananchi wa miradi hiyo baada ya kukamilika. Katika ziara hiyo viongozi wawakilishi wa wananchi, wameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita na juhudu za mhesimiwa Rais, mama Samia Suluhu kwa kuelekeza fedha nyingi, kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za halamshauri ya Arusha, jambo ambalo wamekiri halijawahi kutokae na kuongeza kuwa, fedha hizo za ujenzi wa madarasa zimekuja wakati muafaka kwa kuwa kila mwaka, wananchi hulazimika kuchangishana kujenga madarasa ya kidato cha kwanza kwa mwaka unaofuata.Diwani wa kata ya Bangata Mhe. Ezra Tomito amesema kuwa licha ya kuwa madarsa hayo yatawanufaisha watoto wao, lakini kwa kiasi kikubwa yamewapunguzia wananchi mzigo wa kuchangishana fedha za ujenzi wa madarasa, amabo hufanyika kila mwaka nyakati kama hizo.Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amemshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa kukuabali kupokea na kuzindua vyumba 9 vya madarasa, kama mfano wa madarasa yote yaliyokamilika katika halamshauti ya Arusha, na kumuhakiksihai kuendelelea kusimamia utekelezaji wa majukumu ya serikali ya kuwatumikia wananchi, pamoja na kuyafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo kusimamia fedha zilizoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi katika sekta zote. Katika ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, ametembelea jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi milioni 860, miradi 7 ya sekta ya elimu na mradi mmoja wa upanuzi wa kituo cha Afya Oldonyosmabu unaogharimu shilingi milioni 200.Ikumbukwe kuwa, halmashauri ya Arusha ilipokea shilingi bilioni 2, fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19, za ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa, kwa mgawanyo wa madarasa 96 shule za sekondari na madarasa 4 kwa shule mbili za msingi shikizi, madarasa yote yanatakiwa kujamilika ifikapo 31, Desemba, 2021.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.