• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC GAMBO AITAKA DFID KUENDELEA KUSIMAMIA MRADI WA MAJI WA VIJIJI VITANO ILI UWE ENDELEVU

Posted on: January 29th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, mheshimiwa Mrisho Gambo, ameitaka Idara ya Maendeleo ya nchini Uingereza ' Department For International Development' (DFID) kujipa muda wa kufanya tafiti zaidi ya namna ya kuendesha mradi wa maji wa Vijiji vitano, mara baada ya mradi huo kukamilika na kukabidhiwa kwa serikali, kutokana na gharama kubwa za uendeshaji mitambo ya kuchuja maji, ili mradi huo uwe endelevu kama ulivyokusudiwa.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa rai hiyo  ofisini kwake,  alipokutana na ujumbe kutoka  DFID - Tanzanzia, ujumbe uliolenga kutoa taswira halisi ya utekelezaji wa mradi huo wa maji, unaotekelezwa kwenye vijiji vitano ndani ya halmashauri ya Arusha na shirika la WaterAid Tanzani, kwa gharama ya shilingi bilioni 8.4.

Mheshimiwa Gambo ameweka wazi kuwa, mradi huo wa maji umesanifiwa kwa kutumia mitambo ya kisasa, yenye kuchuja maji na imetumia gharama kubwa, huku uendeshaji wa mitambo hiyo, ukitegemea kutumia gharama kubwa za uendeshaji na kuitaka DFID, kujipa muda zaidi wa kusimamia mradi huo mpaka kufikia hatua ambayo mradi huo utaweza kujiendesha.

"Mradi huu wa maji, umegharimu fedha nyingi na unatumia mitambo ya kisasa ya kuchuja maji, mitambo inayohitaji gharama kubwa za uendeshaji, niombe DFID hata baada ya mradi kukamili, kujipa muda wa  kuendelea kushirikiana na  serikali kusimamia uendeshaji wa mradi huo ili uweze kuwa endelevu" amesema mhe. Gambo

Ameongeza kuwa, wananchi wana maratajio makubwa kwenye mradi huo, kutokana na ukweli kwamba, wananchi hao wameteseka kwa adha ya maji kwa muda mrefu, kutokana na shida ya maji yenye madini ya floraidi, inayowakabili wananchi hao, na kusisitiza kuwa DFID wanapaswa kuangalia umuhimu wa mradi huo kwa wananchi pamoja na gharama kubwa walizotumia kutekeleza mradi huo.

Hata hivyo mwakilishi wa DIFID, Getrude Mapunda, licha ya kuishukuru na kuipongeza serikali kupitia uongozi wa mkoa wa Arusha, ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, halmashauuri ya Arusha na wadau wote wanaotekeleza mradi huo wa maji, amesema kuwa, wataendelea kushirikiana na serikali, wadau na wananchi kuhakikisha mradi huo mkubwa unakuwa endelevu kama ilivyo katika lengo na usanifu wa mradi.

Getrude amefafanua kuwa DFID, inafadhili miradi ya maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wapata maji safi na salama na kuongeza kuwa mradi huo wa vijiji vitano, umesanifiwa kutumia mitambo ya kuchuja maji na kuondoa madini ya floraidi na madini ya chumvi, mitambo ambayo imetumia gharama kubwa, lengo likiwa ni kuwapatia wananchi maji safi na salama na mradi kuwa endelevu.

Naye Mkurugenzi wa shirika la WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole, amemueleza mkuu wa mkoa kuwa, mradi huo ulianza mwaka 2017, kwa sasa uko katikz hatua za mwisho kukamilika, na wanategemea kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Machi, 2020.

Dkt. Kabole amefafanua kuwa mradi huo utakuwa na vituo 92 vya kuchotea maji na tayari vituo 46 vya kuchota maji vimeanza kutoa huduma, huku vituo vingine 41 vikiendelea na ukamilishaji, wakati huo huo, marekebisho madogo madogo yakiendelea kufanyika kabla ya wakandarasi kukabidhi mradi.

Mradi wa maji wa Vijiji vitano, umefadhiliwa na DFID na kutekelezwa na Shirika la WaterAidTanzania, unategemea kukamilka mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu wa 2020, na utahudumia takribani wananchi 50,000 wa vitongoji vya Ngaramtoni, Ekenywa, Seuri na vijiji vya Olkokola na Lengijave, halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.