Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameikumbusha timu ya Menejimenti halmashauri hiyo, kutambua kuwa cheo ni dhamana, hivyo watumishi wanapaswa kutumia dhamana hiyo kwa kuwatumikia wananchi wa halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Msumi, ameyasema hayo, alipokutana kwa mara ya kwanza na timu ya menejimenti ya halmashauri ya Arusha, kwenye kikao mkakati cha wiki mamarufu kama 'morning prayer' ambapo alitumia nafasi hiyo kujitambulisha, timu inayojumuisha wakuu wa Idara na Vitengo, na kuwataka kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuwatumikia wananchi, kwa maendeleo ya halmashauri na taifa kwa ujumla.
Aidha Mkurugenzi Msumi, ameweka wazi kuwa, anazo taarifa kuwa halmashauri ya Arusha, ni moja kati ya halmashauri nchini zinazofanya vizuri katika sekta zote, na kufuatia matokeo mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake, yuko tayari kuyaendeleza kwa kushirikiana na watumishi wote wa halmashauri ya Arusha, kufanya kazi kama timu na kila mmoja kutumia ujuzi alionao kufuatia maekelekezo ya kazi kwa kada husika, huku wakizingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ili kufikia malengo yaliyowekwa.
"Ninaamini kwenye kufanya kazi kwa ushirikiano, kwa pamoja kama timu, mimi ni muumini wa 'team work', mkurugenzi hawezi kufikia malengo kama wakuu wa Idara, wakuu wa vitengo na watumishi wengine hawata nia mamoja, ninachotamani kila mtu awe active, aheshimu wengine, afanye kazi kwa uaminifu na kwa moyo wa uzalendo bila kusukumwa wala kusimamiwa kwa karibu, kwa kuwa kila mtu ana mpango kazi wake na ana malengo yatakayopimwa kwenye mpango kazi huo". Amefafanua Mkurugenzi Msumi.
Mkurugenzi Msumi, licha ya kuwapongeza na kuwashukuru watumishi wa halmashauri hiyo kwa kumpokea, ameweka wazi hisia na matamanio yake, kuwa anatamani watumishi siku moja halmashauri ya Arusha kuwa halmashauri namba moja nchini inayoongoza kisekta katika masuala ya ukusanyaji mapato, elimu afya na maji na maendeleo kwa ujumla.
Hata hivyo, mkurugezi huyo, amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika kupambana na UVIKO 19, kwa kuhamasisha jamii, kufuata maelekezo yanayotolewa na watalamu wa afya ikiwemo, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa, tumia vitakasa mikono pamaoja na kuepuka misongamano.
Naye Afisa Elimu Msingi, mwalimu Hossein Mghewa, aliyekaimu kiti hicho cha ukurugenzi, amemkaribisha mkurugezi Msumi na kumponhez kwa kuteuliwa kwake, kuiongoz halamshauri ya Arusha pamoja na kumuahidi kumpa ushirikiano, kwa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia maono ya halmashauri kwa kuifanya kuwa halmashauri inayoongoza kwa kutoa huduma bora kwa jamii na maendeleo endelevu ifikapo 2025.
Mkurungenzi Msumi, aliyeteliwa tarehe 01.Augosti, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kuwa Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, anakuwa ni mkurugenzi wa sita kuongoza halmashauri ya Arusha, tangu ilipogawanywa iliyokuwa halmashauri ya wilaya ya Arumeru Julai 1, 2007 na kupata halamshauri ya Arusha na Meru, zote zikiwa wilaya ya Arumeru.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akizungumza kwa mara ya kwanza na timu ya Menejimenti inayojumuisha Wakuu wa Idara na Vitengo, kwenye kikao kazi cha wiki maarufu kama 'Morning Parayer', kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.