• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHIRIKA LA AVUREFA KUTOA HUDUMA ZA AFYA ZA MKOBA (MOBILE CLINIC)- ARUSHA DC

Posted on: February 21st, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

Shirika lisilo la kiserikali la Aspiration for Vulnerable Rehabiltated Families (AVUREFA),  litaanza rasmi kutoa huduma za afya za mkoba 'mobile clinic', kwenye maeneo ya pembezoni, katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, lengo likiwa ni kupambana na magonjwa sugu na kuwa na taifa lenye afya bora.

Akizungumza wakati wa kulitambulisha shirika hilo, kwenye kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa SOS, Mkurugenzi wa Shirika la AVUREFA, Dkt. Furaha Kitiwe, amethibitisha kuwa, shirika hilo litaanza kutoa huduma za afya za majumbani, kwa maeneo ya pembezoni kwa kuwahudumia wagonjwa walioathirika na ugonjwa wa UKIMWI na Kifua Kikuu, Utapiamlo, huduma za Afya ya Uzazi na uzazi wa mpango.

"Tutashirikiana na halmashauri kutoa huduma hizo, kupitia 'mobile clinic' kwa kuwafikia watu katika maeneo yao, lengo likiwa ni kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa sugu ya UKIMWI na  TB, Kansa ya Mlango wa kizazi na kutambua dalili za awali, kuwapima, kutibu na zaidi kuzuia maambukizi kutoka kwa mgonjwa  kwenda  kwa mtu mwingine" amesema Mkurugenzi wa AVUREFA.

Aidha, Dkt. Kitili amefafanua kuwa, shirika litashirikiana na watalamu wa afya wa halmashauri hiyo, kuwafikia wagonjwa hao majumbani, na kutoa elimu ya maambukizi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, dalili zake, namna ya kujinga pamoja kuwafanyia vipimo, kutoa dawa, na namna ya kuwatunza wagonjwa hao na kuepuka unyanyapaa na maambukizi mapya pamoja na elimu ya lishe bora kwa wagonjwa hao.

Hata hivyo Dkt. Kitiwe amefafanua kuwa, shirika hilo limeamua kutoa huduma hizo za afya, kwa lengo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika sekta ya afya, hasa katika kuweka mazingira rafiki ya kuwahudumia wananchi  na kuwafikia hasa wa maeneo ya vijijini.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa wilaya, Afisa Afya, halmashauri ya Arusha, Issa Msumari, amesema kuwa, halmashauri itashirikiana na shirika hilo, kuwahudumia wagonjwa hao, majumbani ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya Serikali ya kuwafikia wagonjwa hasa waishio maeneo ya pembezoni.

Ameongeza kuwa lengo la serikali ni, kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili kuweza kufanyakazi na kujenga taifa, kwa kuwapatia elimu ya afya na magonjwa, sambamba na kuwapatia huduma bora za afya, pale wanaposhambuliwa na magonjwa, hivyo shirika hilo linatekeleza malengo halisi ya serikali.

Naye, Afisa Mtendaji wa kata ya Sambasha, Nkini amekiri,  uhitaji wa huduma hizo za afya majumbani, kutokana na uelewa mdogo wa jamii, juu ya ugonjwa Kifua Kikuu na maambukizi,  namna ya kujikinga na namna ya kuwahudumia wagonjwa hao pamoja na lishe bora kwa wagonjwa, jambo ambalo linasababisha ongezeko la wagonjwa na pengine vifo.

"Bado jamii haina uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa wa TB, dalili za ugonjwa huo, kuchelewa kwenda hospitali kupata vipimo, jambo linalosababisha maambukizi kutokea, kupitia huduma hizo, tutaweza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi" amesema Afisa Mtendaji huyo.

Awali, shirika la AVUREFA linaanza kutekeleza mradi huo wa awali kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa, kwa kuanza na kata ya Sambasha na baadaye kuendelea maeneo mengine ya pembezoni ya halmashauri hiyo.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.