• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHIRIKA LA CCS KUANZA MRADI WA KUCHUJA MAJI KIJIJI CHA ENGUTUKOIT KATA YA OLDONYOWAS

Posted on: April 3rd, 2023

Na Elinipa Lupembe

Shirika lisilo la kiserikali la Climate Change Solution (CCS) limejipanga kuanza kutekeleza mradi wa kuchuja maji ili kuondoa madini ya floride kijiji cha Engutukoit kata ya Oldonyowas.

Akiwasilisha mpango wa utekelezaji wa mradi huo, kwa wajumbe wa kikao cha menejiment, kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji halamsahuri ya Arusha, Mratibu wa mradi, Jorg Lenkel amesema kuwa shirika hilo linatarajia kutekeleza mradi huo wa maji unaotarajia kugharimu kiasi cha shilingi milioni 71 fedha za kitanzania.

Amesema kuwa mradi huo utahusisha ukarabati wa miundombinu ya maji iliyopo kijijini hapo, ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 5,000 litakalosimikwa mtambo wa kuchujia maji kupitia madini ya mkaa, pamoja na kiongeza vituo vya kuchotea maji kijijini hapo.

Jorg amesema kuwa lengo la mradi huo, kuweka mfumo utakaowezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa wakazi wa Engutukoit, kutokana na changamoto kubwa inayowakabili wananchi wa eneo hilo ya maji kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya floraidi, madini ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu.

Aidha amefafanua kuwa mradi huo unategemea kutekelezwa kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa na unategemea kuhudumia wananchi wote wa kijiji cha Engutukoit.

Hata hivyo, menejiment ya halmashauri, imepokea kwa mikono miwili mradi huo kutokana na ukweli kuwa, maeneo hayo yana maji yenye kiasi kikubwa cha madini ya floraidi, madini ambayo yana athari kubwa kwa binadamu.

Kaimu mkurugenzi, halmashauri ya Arusha Omary Sembe, amewataka wadau hao kutekeleza mradi huo kwa kuzingatia viwango vya ubora unaoendana na thamani ya fedha, pamoja na kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za nchi ikiwemo mila na desturi za wakazi wa eneo hilo.

Awali shirika la CCS linafanya kazi kwa kushirikiana na shirika la  Oikos East Africa, na kutekeleza mradi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Vijijini RUWASA - ARUMERU kwa ufadhili wa Free State of Saxony kupitia Foundation North South Bridges, the working Group wa nchini Ujerumani.

"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"






Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.