Diwani wa Kata ya Sambasha Mhe. Mosses Ataulwa Lukumai akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata ya Sambasha kwa kipindi ya robo ya nne ya kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2023.
Hata mheshimiwa Mataula ameishukuru serikali kwa kuwapa fedha shilingi milioni 81.3 zilimotekeleza mradi wa ujenzi wa vyumba vya 3 vya madarasa shule ya msingi Timbolo kupitial mradi wa BOOST, lakini zaidi ameiomba serikali kuendelea kutoa fedha za ukarabati wa shule nyingine za msingi katani hapo kutokana na kuwa na miundombinu chakavu iliyojengwa miaka mingi iliyopita.
Aidha amewasilisha changamoto ya ubovu wa miundo mbinu ya barabara na vinvuko vilivyoharibiwa na mvua za masika pamoja na baadhi ya vitongoji kutokufikiwa na umeme wa REA, ambao unaMwkafanya wananchi wake kujisikia wanyonge kwa kukosa nishuati muhimu ya umeme.
tano huo umefanyika kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.