Na Elinipa Lupembe
Jumla ya miradi 4 ya maji imetekelezwa halmashauri ya Arusha kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.7 kwa kipindi cha miezi tatu ya robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji, Meneja wa Wakala wa maji vijijini wilaya ya Arumeru Mhandisi Sabiri Waziri amesema kuwa kiasi hicho cha fedha ni kutoka serikali Kuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya maji pamoja na mradi wa lipa kwa matokeo awamu ya 5.
Ameainisha kuwa shilingi bilioni 1.2 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya maji zimetekeleza miradi 2, mradi wa maji kijiji cha Losikito milioni 550 na mradi wa maji Olmulo shilingi milioni 691.6.
Amefafanua kuwa shilingi milioni 526 fedha za mradi wa lipa kwa matokeo awamu ya 5, milioni 350 zimetekeleza mradi wa maji vijiji vya Manyire - Majimoto - Marurani na milioni 176 zimetumika kukarabati bomba la zamani mradi wa maji Nduruma (old Nduruma)
Ikumbukwe kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata maji ndani ya mita 400 kwenye maeneo wanayoishi, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 - 2025.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tuungane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.