• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TASAF YAWEZESHA KAYA MASIKINI KUWA WAJASIRIAMALI ARUSHA DC

Posted on: July 16th, 2021

Na.Elinipa Lupembe

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii -TASAF kupitia mradi wa mpango wa kunusu kaya masikini, umewawezesha wanufaika wa mpango huo katika halmashauri ya Arusha, kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa kutumia ruzuku ya fedha wanazopata kila baada ya miezi miwili.

Wanufaiko hao wamekutwa na mwandishi wetu wakiendela kufanya biashara nje ya ofisi ya kijiji cha Ilkiding'a, wakati wanasubiri kupokea fedha zao za ruzuku ya TASAF, huku zoezi la uhawilishaji wa fedha za kaya masikini, likiendelea katika ofisi hizo, ikiwa ni ruzuku ya mwezi Mei na Juni 2021.

Waafanyabiashara hao ndogo ndogo wamekiri kuinua biashara zao kupitia fedha ndogo wanayoipokea kama ruzuku ya mpango wa kunusuru kaya masikini, mradi unatekelezwa na serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii -TASAF,  na kukiri kuwekeza fedha hizo kwenye biashara ndogo ndogo kama kuuza mitumba, vyomba na kuuza mbogamboga sokoni.

Loveness Rashid, mkazi wa kijiji cha Ilkiding'a na mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini amethibitisha kupata mtaji wake wa kuuza vyombo, kupitia fedha hizo za ruzuku na kuonheza kuwa japo pesa hizo ni kidogo lakini zinawawezesha kuendesha maisha na kuondokana na umasikini uliokithiti waliokuwa nao hapo awali.

"Ninauza vyombo kama unavyoviona hapa, na wateja wangu ni hawa hawa wanufaika wa mpango wa kaya masikini, tunaishukuru serikali yetu, tunamshukuru mama Samia, kwa kutuwezesha kupata pesa hizi, zimesaidia watu weng hapa kijijinii amabao hawana uwezo na hali duni za maisha, sasa hivi walau wanamaisha mazuri sio kama zamani" amesiaitiza Loveness

Naye Elinita Mollel, mfanyabiashara wa kuuza nguo za mitumba kwa kutembeza mitaani, amesema kuwa mtaji wa biashara hiyo umetokana na fedha za ruzuku ya TASAF, biashara amabyo anaitegemea kuendesha maisha ya familia yake na familia kwa ujumla.

Aidha mnufaika mwingine wa kijiji cha hicho hicho cha Ilkiding'a, na mfanyabiashara ya mboga wa soko la Samunge lajijini Afusha, Felista Moses Laizer, amesema kuwa licha ya kuwa anapokea kiasi kidogo cha fedha, kilimuwezesha kuanza  biashara ya kuuza mboga  sokoni, biashara ambayo imesaidia kumudu kuendesha maisha ya familia yake, huku pato la familia likipanda tofauti na hapo awali ambapo hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya sana.

"Nilipokea hela ya TASAF kiasi nikatumia na shilingi elfu 10, nikatumia kama mtaji wa biashara yangu ya kuuza mboga, nanunua mboga kwa wakulima shambani na kuuza  sokoni, TASAF imenisaidia , sikuwa na uwezo hata wa kupata huo mtaji wa elfu 10,kwa sasa hali ya maisha sio mbaya kama hapo zamani" amefafanua Felista.Hata hivyo Mratibu wa TASAF halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa mpango huo wa kunusuru kaya masikini, umenufaisha familia nyingi ambazo hutumia fedha hizo kufanya biashara ndogo ndogo, tofauti na wale amabao hupoke pesa hizo na kula tu na kuwataka wanufaika hao kuendele kutumia kiasi cha fedha hizo kuwekeza kwenye biashara ndogo ndogo jambo ambalo litarahisisha hali za maisha yao.Mratibu huyyo ameeleza kuwa kwa kipinid cha mwezi Mei na Juni 2021, halmashauri imetoa ruzuku ya takribani shilingi milioni 284.4, kwenye jumla ya kaya 8167 katika vijiji 45 vilivyo kwenye  mpango wa kunusu kaya masikini, mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya III.



Mnufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na mjasiriamali Elinita Mollel akiwa kwenye biashara yake ya kuuza nguo za mitumba, aliyoanzisha baada ya kupokea ruzuku ya TASAF.

Mnufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na mjasiriamali Riziki Naftali, akiwa kwenye biashara yake ya kuuza vyombo, aliyoanzisha baada ya kupokea ruzuku ya TASAF.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.