Na Elinipa Lupembe
Teknolojia ya Uhimilisha inayohusisha upandishaji wa ng'ombe kwa kutumia chupa, imekuwa na mchangi mkubwa katika ufagaji wa kibiashara kwa kuwaongezea wafugaji mazao ya mifugo pamoja na kuwaongezea kipato
Wafugaji halmashauri ya Arusha, wamethibitisha kunufaika na teknolojia hiyo ya uhimilishaji wa ng'ombe, iliyoongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na ng'ombe, yaliyowaongeze kipato cha sambamba na kuwapeleka kwenye ufugaji wa kibiashara.
Wafugaji hao wakiwa wameleta mifugo yao kwenye maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi - Njiro jijini Arusha, wamekiri teknolojia ya kupandisha ng'ombe kwa njia ya chupa imelemeta mapinduzi makubwa katika uzalishaji na ongezeko la mazao ya mifugo.
Regan Laiza, mfugaji kutoka kijiji cha Lemanyata kata ya Lemanyata, amekiri kuwa na mabadiliko makubwa ya uzalishaji mara baada ya kutumizi ya teknolojia ya uhimilishaji, ambayo imeleta mapinduzi kwa wafugaji, kwa kuwa na ng'ombe bora, wanaokua haraka huku wakizalisha maziwa na nyama nyingi zaidi tofauti na hapo awali walipokuwa wanafuga ng'ombe waliozalishwa kwa kuoandishwa.
Amefafanua kuwa wafugaji kwa sasa, wanajivunia teknolojia hiyo, na kumuelezea ng'ombe wake mwenye umri wa miaka 4, ana uzito wa kilo 500 na tayari ana ndama mapacha na mwenye uwezo wa kutoa lita 35 mpaka 40 za maziwa kwa siku, maziwa ambayo yakiuzwa yatampatia wastani wa shilingi elfu 55 kwa siku.
"Ngombe hawa wawili wamepatikana kwa kutumia teknolojia ya Uhimilishaji, aina ya fresian wate wakiwa na uwezo wa kutoa maziwa lita 30 -40 kwa siku, huku maziwa hayo yakiingiza takribani shilingi milioni 15 -20 kwa mwaka" Amebainisha mfugaji Regan
Naye Alfayo Mollel, mfugaji na msindikaji wa bidhaa za maziwa, amebainisha kuwa teknolojia ya uhimilishaji imewapa matumaini wafugaji, na kuongeza kuwa kwa sasa mradi wake wa ufagaji ng'ombe, unajiendesha wenyewe kupitia maziwa yake na kuleta faida kubwa tofauti na ufugaji wa zamani ambapo ng'ombe alitoa lita 3 za maziwa kwa siku.
"Teknolojia hii imeleta matumaini kwetu wafugaji, upatikanaji wa maziwa mengi umeniwezesha kuanzisha kiwanda cha kusindika maziwa na kuliongezea thamani zao la maziwa, kwa sasa ninapark maziwa fresh, mtindi, yoghot, samli na siagi, pamoja na matumizi ya gesi ya kinyesi 'bio gas' ambayo pia nimeanza kuuza kwa majirani zangu" Amefafanua Alfayo
Maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini 2023 mefunguliwa rasmi Agosti 3, yenye kauli mbiu ya "Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo ya chakula", na yanatarajiwa kufungwa mapema Agosti 8, 2023.
Karibu Banda la Mifugo Halmashauri ya Arusha Tukuhudumie✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.