• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

UBALOZI WA JAPANI NCHINI, WAKAMILISHA UJENZI WA MADARASA YA GHOROFA SEKONDARI SEKONDARI SOKON II

Posted on: February 7th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

Ubalozi wa japani nchini Tanzania, umeendelea kushiriki kuchangia sekta ya elimu halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, kwa kujikita katika ujenzi wa miundo mbinu ya shule, ili kuweka mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia kwa  wanafunzi na kupandisha kiwango cha elimu nchini.

Ubalozi huo wa Japani, umefanikisha ujenzi wa msingi wa jengo la ghorofa mbili lenye jumla ya vyumba 12, kati ya vyumba hivyo, tayari vyumba vinne vya madarasa, matundu ya vyoo pamoja na meza na viti 160, katika shule  ya sekondari Sokoni II, vimekamilika, kwa gharama ya shilingi milioni 196.

Akizungumza shuleni hapo jana, Afisa Miradi, Ubalozi wa Japani nchini Tanzania, Ayuni Sakai, amesema kuwa, amefurahishwa sana kuona jengo hilo limekamilika na wanafunzi wameanza kutumia madarasa hayo, jambo ambalo ndilo lengo hasa la ubalozi huo wa Japani nchini na kuahidi kuendelea kushirikiana na halmashauri hiyo, kutekeleza miradi mingine ya kijamii.

"Nimefurahishwa sana na ushirikiano wenu na ukamilishaji wa jengo hili, mmeonyesha jitihada kubwa kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa ubora, nimefurahi zaidi kuona tayari wanafunzi wanafundishwa kwenye mazingira bora wakiwa  na  furaha pamoja na walimu wao"  amesema Ayuni.

Ameongeza kuwa, lengo la Ubalozi huo ni kushirikiana na Serikali ya Tanzania, kuboresha huduma za jamii na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao, na dunia kwa ujumla.

Nao wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Sokoni II, wanaotumia madarasa hayo, wameushukuru Ubalozi huo wa Japani kwa msaada wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, uliowawezesha kufundishiwa kwenye mazingira bora sasa, mazingira ambayo yamewarahisishia tendo zima la kujifunza na kufundishwa na wameahidi kufanya vizuri katika matokeo yao ya mtihani wa taifa wanaotegemea kufanya mwanzoni wa mwezi Novemba 2020.

Josephine Maglani, mwanafunzi wa kidato cha nne, amethibitisha kuwa, yeye na wanafunzi wenzake wanaupongeza Ubalozi huo, kwa kuwajengea madarasa, jambo ambalo ni la maendeleo makubwa shuleni kwao, na kuhaidi kuongeza bidii katika masomo na kupata ufaulu wa kiwango cha juu katika shule yao, kwenye mitihani yao ya  Taifa mwaka huu.

"Mimi na wanafunzi wenzangu, tumefurahishwa na hatua hii ya kimaendeleo shuleni kwetu, kwa kuwa sasa, tunasoma kwenye madarasa mazuri na tunaahaidi kufanya juhudi na kufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili" amesema Josephine"

Mkuu wa shule ya Sekondari Sokon II, mwalimu Mwamvita Kilonzo, licha ya kuushukuru Ubalozi huo wa Japani, amethibitisha kuwepo kwa changamoto kubwa ya uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo, changamoto inayotokana na ongezeko kubwa la wanafunzi, tangu serikali ya awamu ya tano, kuanza kutoa elimu bila malipo.

Ameongeza kuwa, mradi huo umesaidia  kutatua changamoto ya uhaba huo, kwa kiasi kikubwa, kutokana na ukweli kwamba, Januari mwaka huu 2020, wamepokea jumla ya wanafunzi 314 wa  kidato cha kwanza na endapo madarasa hayo yasingejengwa, wanafunzi hao wangekosa mahali pa kusomea.

" Kukamilika kwa madarsa haya, kumetusaidia sana kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa, kwani hatukuwa na madarasa ya kutosha kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu.

Awali, ujenzi wa jengo hilo ulianza mapema mwezi Machi 2019 na kukamilika mwishoni mwa mwaka huo, hata hivyo ubalozi huo wa Japani, umekuwa na ushirikiano mkubwa wa kimaendeleo na halmashauri ya Arusha, mpaka sasa umeweza kujenga miundombinu ya shule za Sokoni II na Enyoito pamoja na ukamilishaji wa Kituo cha Afya Manyire.










Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.