• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

UBALOZI WA JAPANI WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA SOKONI II SEKONDARI

Posted on: October 1st, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, umeridhishwa na uyekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Sokon II, halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru.

Akizungumza na mwandishi wetu, Mratibu wa Miradi kutoka Ubalozi wa Japan, nchini Tanzania, Ayumi Kasai, alipotembelea na kukagua mradi huo, amethibitisha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japani nchini.

Ayumi amesema kuwa, licha ya kuwa ujenzi huo, umeanza mwezi Mei 2019,  mpaka sasa umeekamilika kwa zaidi ya asilimia 55 jambo ambalo linatia moyo na kuleta matumaini ya kukamilika kwa wakati kulingana na mkataba wa ujenzi.

Hata hivyo Ayumi ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Arusha kwa ujumla wake, kwa usimamizi imara wa miradi na kuongeza kuwa, kutokana na ushirikiano wa Ubalozi wa Japani na halmashauri ya Arusha, Ubalozi huo umejipanga kuendelea kutekeleza mradi mwingine ndani ya halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Elimu Taaluma, halmashauri ya Arusha, John Charles, amesema kuwa, halmashauri inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Ubalozi wa Japani, hasa katika sekta ya Elimu, sekta ambayo ni nyeti kwa manufaa ya Taifa la Tanzania na vizazi vyake.

Ameongeza kuwa, halmashsuri itahakikisha mradi huo, unakamilika kwa wakati, na madarasa hayo kuanza kutumika, madarasa ambayo yanategemewa kupunguza, msongamano wa wanafunzi unaosababishwa na uhaba wa vyumba vya madarasa uliopo shuleni hapo kwa sasa.

"Nikuhakikishie kuwa, ujenzi huu utakamilika kwa wakati, na wanafunzi wataanza kuyatumia ndani ya mwaka huu, na kupunguza msongamano wa wanafunzi uliopo kwa sasa" amesema Charles.

Naye mkuu wa shule ya Sekondari Sokon II, mwalimu Mwamvita Kilonzo, amesema kuwa, vyumba hivyo vya madarasa vitachukua jumla ya wanafunzi 180 kwa uwiano wa wanafunzi 45 kwa darasa moja.

Ameongeza kuwa, shule ya Sokoni II ina vyumba 11 vya madarasa ikiwa na uhitaji wa vyumba 11 zaidi, ikiwa na jumla ya wanafunzi 993, na kuongeza kuwa kukamilika kwa vyumba hivyo vinne, vitaongeza idadi na kubakiza upingufu wa vyumba saba.

Ubalozi wa Japani nchini Tanzania, umetoa fedha kiadi cha shilingi milioni 195, kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa ghorofa na ukamilishaji wa vyumba vinne vya madarasa,  vyoo vya wanafunzi pamoja na samani za madarasa yote, mradi ulionza kutekelezwa mwezi Mwei 2019 na unategemea kukamilika mapema ifikapo mwezi wa Oktoba 2019.


Mratibu na msimamizi wa Miradi, Ubalozi wa Japani, Ayumi Kasai, akikagua ramani ya Jengo la ghorofa vyumba vinne vya madarasa shule ya sekondari Sokon II, kulia ni Mhandisi wa Idara ya Ujenzi, Mhandisi  Bibie Manzi.


Mratibu na msimamizi wa Miradi, Ubalozi wa Japani akikagua ujenzi wa Jengo la ghorofa vyumba vinne vya madarasa shule ya sekondari Sokon II.


Muonekano wa Jengo la ghorofa vyumba vinne vya madarasa shule ya sekondari Sokon II.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.