• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

UJENZI WA VYUMBA 100 VYA MADARASA YA UVIKO 19, WAANZA KWA KASI ARUSHA DC

Posted on: November 7th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa halmashauri ya Arusha umeanza kwa kasi, ukiwa katika hatua za awali kutegemea na maeneo, huku asilimia kubwa wakiwa kwenye hatua ya msingi na maeneo mengine wakiwa wameanza kupandisha kuta.

Utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa kujengwa kwa wakati mmoja, mradi ambao haujawahi kufanyika, tangu kuanzishwa kwa halmashauri ya Arusha, unatekelezwa kufuatia fedha za mgao wa kutoka serikalini kuu, kwa ajaili ya mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Naye Kurugenzi Mtendaji, halmasahuri ya Arusha, Seleman Msumi, amesema kuwa ujenzi huo umeanza kwa kasi, katika shule zilizopokea fedha hizo, ukitumia mfumo wa 'force akaunti', na kuahidi kusimamia utekeleza wa mradi huo kwa weledi, ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha, kama ilivyo agizo la serikali la kukamilisha mradi huo kabla ya tarehe 15, Desemba 2021.

Naye Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwalimu Menard Lupenza, ameutaja mgao huo wa vyumba 100 vya madarasa katika halmashauri hiyo, kuwa jumla ya vyumba 96, vinajengwa kwenye shule zote 30 za sekondari za serikali, huku shule 2 za msingi shikizi zikijengwa vyumba 4 vya madarasa, mradi unaogharimu kiasi cha  shilingi bilioni 2, ikiwa na mgawanyo wa shilingi milioni 20 kwa kila darasa.

"Mgao huo wa idadi ya vyumba vya madarasa, umezingatia upungufu wa vyumba vya madarasa uliokuwepo, kwa ulinganifu wa idadi ya wanafunzi katika shule husika, huku shule ya sekondari Kiranyi ikipata idadi kubwa kuliko shule zote, ikiwa na jumla ya  vyumba 13, ikifuatiwa na shule ya sekondari Ilkiding'a, vyumba 11 na shule ya sekondari Mringa ikijengwa vyumba 10". ameweka wazi Afisa Elimu huyo.

Mkuu wa shule ya sekondari Mringa, Mwalim Salum Magaka, amesema kuwa, shule hiyo inatekeleza mradi wa ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa kwa gharama ya shilingi milioni 200, fedha za mapambano dhidi ya UVIKO 19 na kuongeza kuwa ujenzi wa vyumba hivyo vyote uko kwenye hatua ya msingi na unategemewa kukamilisha kwa wakati na kwa ubora.

"Tunaamini tutakamilisha mradi huu kwa wakati, kwa kuwa tayari tumeshanunua vifaa vyote vya muhimu vinavyohitajika, tumepokea 'materials' yote, kazi iliyobaki hapa ni usimamizi, kumsimamia fundi kwa kuzingatia hatua zote za ujenzi, ili kukamilisha madarasa yote 10, kwa wakati na kwa  ubora unaoendana na thamani ya fedha" amesisitiza mkuu huyo wa shule.

Awali halmashauri ya Arusha, imepata mgao wa shilingi bilioni 2 kutoka shilingi trillioni 1.3 za mkopo wenye riba nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani - IMF, ikiwa ni fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 96 vya madarasa shule za sekondari na Vyumba 4 vya madarasa shule 2 shikizi za Msingi.

 ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍

PICHA ZA HATUA MBALIMBALI ZA UJENZI.














Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.