• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIJANA ARUSHA DC WANUFAIKA NA MIKOPO YA SERIKALI ISIYOKUWA NA RIBA

Posted on: February 5th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

Serikali ya awamu ya tano, imeendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa vijana wa kitanzania, kwa kuweka mazingira rafiki ya kujiajiri, kwa lengo la kuwakwamua vijana kutoka katika wimbi la umaskini linalowakabili, kuelekea  uchumi wa kati, kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu kupitia asilimia kumi ya mapato ya halmashauri.

Kwa kipindi cha miaka minne ya awamu ya tano, Halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa halmashauri inayotekeleza kwa kasi adhma hiyo ya serikali, kwa kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi milioni 756, ikiwa milioni 156 kwa vikundi 52 vya vijana, milioni  600 kwa vikundi 206 vya wanawake na milioni 10.6 kwa vikundi 4 vya walemavu, mikopo ambayo imewawezesha wanufaika wengi kujikwamua kiuchumi.

Kikundi cha vijana cha 'Umoja Youth Group'  kilichopo kata ya Moivo, ni kikundi kilichonufaika na mikopo hiyo, kinachojihusisha na uchomeleaji vyuma, pamoja na biashara ya kuuza bidhaa za vyuma kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo samani za aina zote na vifaa vya ujenzi.

Kamati ya Siasa wilaya ya Kichama Arumeru, imetembelea na kujionea shughuli zinazofanya na kikundi hicho cha vijana, kikundi ambacho kinaonesha matokeo chanya ya adhma ya serikali ya awamu ya tano, ikiwa ni utekelezaji Ilani ya Chama cha Mapinduzi iliyonadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Akisoma taarifa ya kikundi hicho, Mweka Hazina wa Kikundi, Tito Joakim, amesema kuwa kikundi chao kina vijana watano, na walipata mkopo kutoka serikalini kiasi cha shilingi milioni 10, mkopo ambao licha ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi, umewezesha biashara yao kukua na kujitanua kimasoko, ikiwa ni pamoja na kukidhi mahitaji ya wateja wao kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora zaidi ya hapo awali walipokuwa na mtaji mdogo.

Amesema kuwa, kabla ya kupata mkopo huo, walikua na mtaji wa shilingi milioni 11 tu, mtaji ambao waliupata kwa kuwekeza fedha na kukopeshana kwa riba,  mtaji ambao ulimudu kuwa na vifaa vichache vya kuchomele, na kuongeza kuwa, baada ya kupata mkopo, waliweza kununua mashine 5 za kuchomelea, mashine ya kupakia rangi, vifaa ambavyo vimeongeza ufanisi wa kazi yao pamoja na kuongeza uzalishaji wa bidhaa, kutoka kutengeneza  samani na kuanza kutengeneza bidhaa za ujenzi, na kukidhi soko la wateja wao kwa wakati.

"Awali mtaji wetu ulikuwa mdogo, tulikuwa na mashine moja ya kuchomea, jambo ambalo lilichelewesha utengenezaji  wa bidhaa na kukamilisha kwa wakati,  kwa sasa tuna mashine tano, zinazowezesha kutengeneza bidhaa nyingi kwa wakati mmoja, tulipaka rangi kwa mkono, kwa sasa tuna mashine 5 za kuchomelea,  compressor  ya kupakia rangi, kwa pamoja tunazalisha bidhaa kwa wingi na zenye ubora wa kukidhi mahitaji ya wateja wetu" amesema Joackim

Aidha, kikundi hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi,  kwa kutumia karakana yao kuwafundisha vijana wengine ufundi wa kuchomelea vyuma bila malipo yoyote, mpaka sasa jumla ya vijana wanne kati ya nane waliopata mafunzo hayo wameweza kujitegemea, huku vijana wengine wanne wakiendelea kufanya kazi kiwandani hapo.

Erick Jonathan (17) na muhitimu wa kidato cha nne, amesema kuwa, baada ya kumaliza kidato cha nne, hakupata nafasi ya kuendelea na masomo na kuamua kutumia fursa iliyotolewa na Kikundi cha Umoja, kujifunza ufundi wa kuchomelea, jambo ambalo amekiri kumuwesha kutimiza ndoto zake, zilizoanza kufifia baada ya kushindwa kurndelea na masomo ya kidato cha tano.

"Kikundi hiki cha Umoja Youth Group kimeninufaisha sana kwa kupata elimu bure ya ufundi na nikaweza kujikwamua kiuchumi kwani sasa hivi, nimekua fundi mzuri tuu wa kuchomelea vyuma vya magari pamoja na vitanda vya chuma" amesema Jonathan

Naye Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Arumeru, Simoni Ole Saning'o licha ya kuridhishwa na utendaji wa kikundi hicho, hakusita kuwapongeza vijana hao na kusema kuwa, kitendo walichofanya vijana hao, ndio adhma halisi ya serikali ya awamu ya tano na Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ikiwa na lengo hasa la kuwawezesha  vijana kujiajiri na kuweza kujikwamua kiuchumi, na amewataka wananchi kununua bidhaa kutoka kwa vijana  hao pamoja na kuwawezesha kupata vigezo vya kupata zabuni za Serikali.

"Nimefurahi kukuta kikundi cha vijana kilichopata mkopo usio kuwa na riba  na kuweza kujiendesha kwa kasi kubwa, jambo ambalo vijana wengi hawawezi, niwatake watanzania wenzangu tununue bidhaa kwa vijana hawa ili kuwawezesha kufikia ndoto zao." Amesema Mwenyekiti Saning'o.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mhe. Jerry Muro, ameahidi kuendelea kuvilea vikundi vya vijana ambavyo vimepata mkopo na kujituma kufanyakazi kwa bidii na kuwataka vijana wengine kuiga mfano wa vijana hao, kwa kuchangamkia fursa hiyo adhimu ya Serikali,  huku akiwaonya vijana kuacha uvivu na kukaa vijiweni na kulalamikia serikali bila kufanyakazi.

Ameongeza kuwa, Serikali imetoa fursa ya mikopo  sawa kwa vijana na wanawake lakini vijana hawajitokezi kukopa, jambo linalosababisha pesa nyingi  kukopeshwa vikundi vya wanawake zaidi, huju vijana wakiendelea kukaa vijiweni na kulalamikia Serikali haitoi ajira.

"Serikali inatoa mikopo asilimia 4 kwa wanawake na asilimia 4 kwa vijana, matokeo yake, vijana wanajitokeza kwa uchache sana, na wengine wakipewa mikopo wanatumia tofauti na malengo waliyoainisha, jambo linalowafanya kushindwa kurejesha kwa wakati, na kujikuta wameingia kwenye mgogoro wa madeni, nawaambia vijana wangu, acheni uvivu kuweni serious, fanyeni kazi, serikali ya Magufuli ni ya kazi na si ya maneno, tumia fursa zilizopo kujiajiri" amesisitiza mheshimiwa Muro

Kikundi cha Umoja Youth Group, kilianza kwa kuchanga fedha kwa kuwekeza na baadaye kubuni mradi wa kuchomelea vyuma, na kuanzisha kiwanda kidogo cha kuchomelea vyuma na kutengeneza bidhaa za chuma na baadaye kukopa Serikalini, mpaka sasa kikundi kimeweza kukuza mtaji na kuwafanya vijana hao kujiajiri, kuweza kujitegemea na kujikimu kimaisha.








Katibu wa Kikundi cha Umoja Youth Group  Tito Joackim akisoma taarifa ya Mradi wao wa

Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.