Na Elinipa Lupembe
Wajumbe wa baraza la madiwani halmashauri ya Arusha, wameiomba serikali kufanya ukarabati wa dharura kwenye barabara zilizoharibika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika msimu huu wa masika.
Wajumbe hao wametoa rai kwa serikali, mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TARURA Arumeru kwa kipindi cha robo ya tatu ya Januari - Machi, 2023, kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Waheshimiwa madiwani hao, wameweka wazi kuwa licha ya wananchi kupoteza mali na wengine makazi, lakini kumetokea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara ikiwemo mitaro kujaa tope, barabara kukatika na kusabisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Diwani wa kata ya Olmotony Mhe. David Kinisi, ameweka wazi kuwa, licha ya kuwa serikali ilitengeneza barabara hizo, lakini kutokana na mvua zilizonyesha, kumetokea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, na kuiomba serikali kupitia TARURA, kuweka mipango ya kufanya ukarabati wa barabara hizo ili ziweze kutipitika na kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo.
"Licha ya kwamba Halmashauri kwa kushirikiana na TARARU imechukua hatua za awali za kuzibua mitaro na kuweka vivuko vya dharura, tunaimba serikali kutafuta ufumbuzi wa namna ya kuyameneji ili na kupata suluhisho la kudumu la kuzia uharibu mkubwa kipindi cha mvua". Amebainisha Mhe. Joseph Tinayo, Diwani wa kata ya Olturumet.
Naye Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Arumeru, Mhandisi Mohamed Bakari, amesema kuwa tayari ofisi yake imeainisha mtandao wa barabara zilizoharibika na kuziwasikisha Serikali Kuu, kupitia ofisi ya waziri mwenye dhamana, kwa ajili ya kuomba fedha za dharura, pindi msimu wa mvua utakapopita ziweze kufanyiwa matengenezo.
Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji,halmasahuri ya Arusha, Seleman Msumi, ameyataja maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua zinazoendelea kunyesha na kuharibu miundombinu ya barabara ni pamoja na kata ya Oloirien, Olturumet, Olmotony, Kimnyaki na Sambasha.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.