• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wakazi mkoa wa Arusha watakiwa kuotesha miti kwa wingi kurejesha Arusha ya Kijani

Posted on: April 2nd, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amewataka wakazi wa mkoa huo,  kuotesha miti kwa wingi, ili kutunza mazingira yanayowazunguka na yale ya vyanzo vya maji, kwa lengo la kurejesha uoto wa asili ambao tayari umeharibiwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi.

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa Juma la kupanda miti kitaifa, mkoa wa Arusha, uliofanyika katika shule ya sekondari Ekenywa, kijiji cha Osunyai kata ya Olturoto mapema jana, Gambo amewataka wakazi wa mkoa huo, kuchukua tahadhari na kuanza juhudi za kurejesha uoto wa asili wa mkoa huo kwa kuotesha miti kwa kasi kubwa.

Amewasisitiza wakazi hao, kuifanya Arusha kuwa ya kijani, kama kauli mbiu inavyosema, 'Arusha ya Kijani inawezekana'  kwa kila mmoja katika eneo lake kuhakikisha anapanda miti, na kuirejesha Arusha kwenye asili yake ya kijani kwa vitendo.

"Endapo kila mkazi wa mkoa wa Arusha atapanda miti na kuitunza Arusha itakua ya kijani na uoto wa asili ulioharibika utarejea kama ilivyokua hapo awali" amesema Gambo

Aidha amewakumbusha wananchi kutambua kuwa, ukataji wa miti ovyo unasababisha ukame na vyanzo vya maji kupungua na hatimaye kukauka, madhara ambayo tayari yameanza kuoneka na kuwataka wananchi wote kuchukua tahadhari kwa kuotesha miti kwa kasi kubwa na kwa wingi zaidi.

Wiliam Kivuyo mkazi wa kijiji cha Osunyai kata ya Olturoto, ameiomba serikali kupitia halmashauri ya Arusha, kuzuia uvunaji miti holela kwa kuwa ndio chanzo cha kuruzorotesha  juhudi za upandaji miti zinazofanywa kila mwaka.

"Wako watu ambao hukata miti kwa kutumia mashine (Cheinsaw) ambayo hukata miti mingi kwa muda mfupi, hii ndio inarudisha nyuma zoezi hili linalofanyika kila mwaka na kuhatarisha mazingira yetu" amesema Kivuyo.

Naye mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, ameahidi kusimamia utunzaji wa miti hiyo iliyooteshwa na kuwataka wananchi kuendelea kuitunza miti waliyopanda kwa mikono yao, ili hapi badaye iweze kuwa kumbukumbu ya kihistoria ya kujivunia katika maisha yao.

Uzinduzi wa juma la  kupanda miti kitaifa mkoa wa Arusha, ulinakshiwa na kauli mbiu ya 'Arusha ya kijani inawezekana tupande miti kwa maendeleo ya viwanda', halmashauri ya Arusha inategemea kupanda jumla ya miti 6,000 kupitia wananchi, mashirika na taasisisi za binafsi na zile za serikali.


PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA UZINDUZI WA JUMA LA KUOTESHA MITI MKOA WA ARUSHA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo akijiandaa kupanda kupanda mti kama ishara ya kuzindua Juma la kuotesha miti kitaifa mkoa wa Arusha.


Askofu mkuu wa KKT Jimbo la Kaskazini Kati Dkt.... akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Juma la kuotesha miti kitaifa mkoa wa Arusha.


Diwani wa kata ya Olturoto mheshimiwa Baraka Simon akipanda mti kwenye uzinduzi wa Juma la kupanda miti kitaifa mkoa wa Arusha.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.