Na Elinipa Lupembe
Wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga halmashauri ya Arusha, wameanza kunufaika na programu ya Anzia Sokoni Malizia Shambani kwa Kipato zaidi, mradi unayotekelezwa na shirika la TANSHEP kwa ufadhili wa JICA.
Wakulima hao wamethibitisha hayo, walipotembelewa na mwandishi wetu kwanye mashamba yao katika kata za Bangata na Shambasha na kujionea hali halisi ya kilimo biashara kinachofanywa na wakulima hao.
Neema Mathayo, mkulima mbogamboga kijiji cha Midawe kata ya Bangata amesema kuwa walipata mafunzo ya kufanya tafiti za kuanzia sokoni kutafiti bei za mazao kwa msimu husika kabla ya kuamua kulima zao flani, ndipo hali ya kilimo ilipoanza kubadilika kwa na kuwa kilimo biashara kwa uhalisia wake.
"Hapa tumelima viazi, kwa kufanya tafiti wa soko kabla ya kulima, pindi tutakapovuna uhitaji wa viazi utakuwa mkubwa na bei yake itakuwa kubwa pia, kwa kuwa tumelenga msimu mzuri kwa soko" Amesema Neema
Mzee Joel Labarani, ameweka wazi kuwa programu ya anzia sokoni, imewafanya wakulima kulima kilimo cha kisasa kinachoendana na mahitaji ya soko, na kuwaondoa kwenye kilimo cha mazoea cha kulima tuu ilimradi umeotesha mazao shambani.
Naye Dina Erasto mkulima kwa kata ya Sambasha, amesema kuwa progamu ya anzia sokoni malizia shambani, imeanza kuwaondoa madalali wa mazao ambao waliwanyonya kwa muda mefu, na kuongeza kuwa wakulima sasa wanayomawasiliano ya moja kwa moja na wafanyabiashara sokoni, hivyo mkulima anaamua kumuzia dalali ama kwenda sokoni moja kwa moja kwa kuzingatia bei halisi ya soko.
Hata hivyo Ester Michael, ameishukuru serikali kupitia watalamu wa kilimo ngazi ya kata na halmashauri ya Arusha kwa kuwa na wakulima bega kwa bega, kuwapa ushauri wa kitaalamu pamoja na kuwaunganisha na wadau wengine wa kilimo, masoko na ujasiriamali, unaowawezesha wakulima kuendelea kufanya kilimo biashara.
Awali Mkuu wa Kitengo cha Kilimo, halmashauri ya Arusha, Bahati Mtweve, amesema kuwa programu hiyo ya anzia sokoni malizia shambani kwa kipato zaidi ni utekelezaji wa mkakati wa serikali wa Agenda 10, 30 ya kilimo biashara.
"Kwa sasa wakulima wameanza kunufaika na kilimo, kwanza kwa kulima zao kulingana na mahitaji ya soko na pia kuuza mazao yao kwa kuzingatia bei ya soko bila kunyonywa na wachuuzi ambao walinufaika sana na jasho la mkulima". Amefafanua Afisa Kilimo Bahati
Halmashauri ya Arusha kupitia Idara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaendelea kutoa mafunzo ya utalamu wa kilimo kwa wakulima husasani kilimo cha kisasa kitakachowaletea kipato zaidi na kufikia Agenda 10/30 ya Kilimo Biashara.
"ARUSHA DCNi Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.