• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAKUU WA SHULE WAFUNDWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ARUSHA DC

Posted on: April 24th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Wakuu wa shule nane za sekondari na msingi, halmashauri ya Arusha, waliopokea fedha zilizotolewa na serikali kuu, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika shule zao, wametakiwa  kusiimamia vema matumizi ya fedha hizo, katika utekelezaji wa miradi iliyoelekezwa kwenye shule zao,  kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za Umma.

Rai hiyo imetolewa na Mkururugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, wakati  kikao kazi cha maelekezo ya namna bora ya usimamizia na matumizi ya fedha hizo za serikali, katika kutekelza miradi ya maendeleo, kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 600, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya mendeleo kwenye sekta ya Elimu, hivyo amewaasa wakuu hao wa shule, wakiwa ndio wasimamizi wakuu wa fedha hizo, wanalo jukumu la kusimamia utekelezaji wa fedha hizo, ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa kuzingatia vigezo vilivyotolewa na serikali.

Amefafanua kuwa, lengo la serikali kutoa fedha hizo ni kuboresha miundo mbinu ya shule na kuwezesha mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia shuleni, kwa adhma ya  kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi, na kuongeza kuwa ni jukumu la wakuu hao wa shule, kusimamia vema miradi hiyo ili kuendana na malengo ya serikali kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

"Serikali imetoa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kwa kutumia mafundi wazawa na kutumia rasilimali zinazopatika ndani ya eneo husika yaani 'forced account', nendeni mkasimamie miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa, hakikisheni miradi inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya fedha, kwa kufanya hivyo, serikali itatoa  miradi mingine, ambayo itatatua changamoto za miundombinu inayozikabili shule zetu,  hii ni kwa manufaa ya shule zetu  na maendeleo ya wananchi wa halmashauri yetu" amesisiatiza Mkurugenzi Mtambule.

Naye Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio, amesema kuwa fedha hizo, kiasi cha  shilingi milioni 600, zimepangwa kutumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule saba, ikiwa shule tatu  za msingi na shule nne za sekondari, pamoja na mabweni manne kwa shule mbili za sekondari za kata.

"Serikali Imeelekeza fedha kwenye shule 7 na kila shule itajenga vyumba viwili vya madarasa pamoja na samani za madarasa hayo, kwa shilingi milioni 40 kwa kila madarasa mawili ya shule husika, na upande wa fedha za  ujenzi wa mabweni, yatajengwa kwenye shule mbili za sekondari za kata na kila shule itaajenga mabweni mawili kwa shilingi milioni 160 kwa kila shule". Amesema Afisa Mipango huyo.

Aidha Afisa Mipango Anna, amezitaja shule zitakazotekeleza miradi ya  ujenzi wa madarasa na samani ni pamoja na  shule za msingi  Kambi ya Maziwa, Ilboru na Olimringaringa, huku shule za sekondari zikiwa ni Kiranyi, Kiseriani, Likamba na Iking'a, na kuongeza kuwa mabweni manne yatajengwa katika shule za sekondari Einoti na Mwandeti.

Hata hivyo, walimu hao, licha ya kuishukuru serikali kwa kutoa fedha katika shule zao lakini pia wameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo, kwa kuwapa ujuzi na maaarifa ya matumzi ya fedha hizo za serikali  na namna bora ya kutekeleza miradi hiyo, na kuahidi  kusimamira miradi hiyo kwa ufanisi zaidi, hasa kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha hizo za serikali, huku wakiweka mbele uzalendo kufuatia malengo ya serikali ya kuboresha miundombinu ya shule zao.

Mkuu wa shule ya sekondari Ilkiding'a, mwalimu Supeet Sailevu, ameweka wazi kuwa, shule yake inakabiliwa na changamoto upungufu wa vyumba vya madarasa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga shuleni hapo, na kusisitiza kuwa, anayosababu kubwa ya kutekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa, kulinga na thamani ya fedha zilizopangwa shuleni hapo.

"Fedha hizo ni muhimu sana kwa shule ya Ilkiding'a, kwa kuwa kuna upungufu wa vyumba nane vya madarasa, huku shule hiyo ikiwa na jumla ya wanafunzi 1,428  yenye kuhitaji vyumba 28 kati ya vymba 19 vilivyopo sasa, hizo milioni 53.2 zitatumika kujenga vyumba viwili na samani zake kwa gharama ya shilingi milioni 40, na shilingi milioni 13.2 kwa ajli ya ujenzi wa choo chenye matundu 12". Amefafanua Mkuu huyo wa shule

Miradi hiyo itatekelezwa katika shule za msingi  Kambi ya Maziwa, Ilboru na Olimringaringa, shule za sekondari Kiranyi, Kiseriani, Likamba,  Einoti na Iking'a, shule hizo zote zitatekeleza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na samani zake, huku shule ya sekondari Ilkiding'a ikitekeleza mradi wa vyumba ipviwili vya madarsa na choo.



PICHA ZA KIKAO KAZI CHA MKURUGENZI NA WAKUU WA SHULE













Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.