• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Walimu Sekondari Arusha DC wakumbushwa kufundisha kwa bidii

Posted on: September 17th, 2019

Waalimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuendelea kujituma na kujitolea katika kufundisha kwa bidii ili kufikia malengo ya serikali ya ufaulu wa zaidi ya asilimia 80% kwa kidato cha nne na asilimia 100% kwa kidato Cha pili.

Akizungumza na walimu wa sule ya sekondari Mlangari, alipotembelea shule hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Afisa Elimu Sekondari, Halmashauri ya Arusha Mwl. Menard Lupenza, amewataka waalimu kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kuweka mbele uzalendo zaidi, ili wanafunzi waweze kuelewa wanachofundishwa na kupandisha kiwango cha taaluma kinachokwenda sambamba na ongezeko la ufaulu.

Ameongeza kuwa, licha ya changamoto zinazokabili tendo la kufunisha na kujifunza,  mwalimu anapaswa kutumia ujuzi na maarifa yake yote, vinavyoambatana na mbinu na zana halisi za kufundishia ili kumfanya mwanafunzi kuelewa na kuwa na kumbukumbu za kutosha kwa kitu alichofundishwa.

"Mwalimu unapokuwa darasani unatakiwa kuacha changamoto zote nje ya mlango wa darasa, na kutumia ujuzi, maarifa na mbinu shirikishi wakati wote, bila kusahau matumizi ya zana halisi za kufundishi, jambo litakalorahisisha uelewa kwa wanafunzi pamoja na kumbukumbu " amesema Afisa Elimu huyo.

Aidha Afisa Elimu huyo, amewataka waalimu hao kufanyakazi kwa kushirikiana pamoja na kuheshimu sheria na taratibu zote za kazi na kutambua wajibu na majukumu yao ni kifundisha, na kuifanya kazi hiyo kwa weledi kwa kutumia rasilimali zilizopo, ili shule hiyo iweze kushika nafasi za juu kwenye mitihani ya kitaifa.

Hata hivyo, Afisa Elimu Vifaa na Takwimu, Idara ya Sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwalimu Charles John, amewasihi wanafunzi kuweka jitihada zaidi kwenye masomo yao, na kutambua kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa kuwapatia elimu bila malipo, hivyo ni vema kutumia vizuri fursa hiyo adhimu waliyoipata, kwa kuwa haitarudi tena, waweze kujikomboa kifkra na kimaisha hapo baadae.

Naye mwalimu Kajiru Malaji, amesema kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na walimu za kuwafundisha wanafunzi wao, changamoto kubwa ni upungufu wa mabweni  na wazazi kushindwa kuchangia chakula cha mchana kwa ajili ya watoto wao wawapo shule, jambo linalofifisha matokeo mazuri kwa shule hiyo.

Amewataka wazazi kuona umuhimu wa kushirikiana na walimu kwa kuhakikisha kila mtoto anapata chakula cha mchana awapo shuleni, pamoja na ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu, jambo litakalopandisha kiwango cha taaluma shuleni hapo.

"Wapo wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kuja na kurudi shule, wapo watoto ambao wazazi hawachangii chakula cha watoto wao na kuwafanya kushinda njaa, jamba ambalo huathiri tendo la lujifunza kwa wanafunzi hao" amesema mwalimu Malaji.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mlangarini, wameahidi kutumia fursa waliyonayo kusoma kwa bidii, na kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mitihani yao, kuanzia mitihani ndani, ya kiwilaya, mkoa mpaka Taifa.

Queen Benaford mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule hiyo licha ya kushukuru uongozi wa Halmashauri hiyo kuwatembelea, na kuwakumbusha wajibu wao kama wanafunzi na kuahidi kufanya jitihada kwenye masomo yao na kuhakikisha wanafaulu mitihani yao kuanzia mitihani ya ndani mpaka ile ya kitaifa.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.