• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WA KATA YA KIUTU WAJITOKEZA KUSAFISHA ENEO LA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI YA KATA YAO

Posted on: March 26th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Wananchi wa kata ya Kiutu halmashauri ya Arusha, wamejumuika kwa umoja wao, bila kujali rika wala jinsia zao, wakiwemo wazee, vijana na wanawake, kusafisha eneo lenye ukubwa wa takribani mita za mraba 1,777.5, eneo lililotolewa na wananchi wa kata hiyo, kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata, iliyopewa jina la Kiutu Secondary School.

Wananchi hao wamefikia uamuzi wa kujitokeza  kulisafisha eneo hilo, ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa shule hiyo, mara baada ya Serikali  kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 470, kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari Kiutu, na wananchi wenzao kutoa eneo hilo, kata ambayo haijawahi kuwa na sekondari tangu kupatikana na kwa Uhuru wa Tanganyika.

Wananchi hao, wameweka wazi hisia zao za furaha, huku wakimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan, kwa kusikia kilio chao cha muda mrefu kwa kuwapatia fedha hizo za ujenzi wa shule ya sekondari katika kata yao, kata ambayo haikuwahi kuwa na shule ya sekondari, licha ya kwamba mpango wa serikali ni kuwa na shule ya sekondari kwa kila kata.

"Tunamshukuru na kumpongeza sana mama Samia kwa kutuona sisi wananchi wa Kiutu, kwa miaka mingi sasa, tumekuwa tukichangia fedha za ujenzi wa madarasa kwenye shule zilizopo kwenye kata nyingine, mpaka ilifikia mahali ambapo tulikata tamaa ya kuendelea kutoa michango kwenye shule hizo,  huku watoto wetu wakipata tabu kufuata elimu ya sekondari kwenye kata hizo, kwa sasa tunaamini watoto wetu hawatanyanyasika tena, watasoma hapa hapa nyumbani" wamesisitiza wananchi hao

Wananchi hao zaidi wamewashukuru wananchi wenzao wanne wenye imani na moyo wa kipekee na uzalendo, kwa kutoa eneo hilo, huku shukrani zaidi zikielekezwa kwa Mheshimkwa Diwani wa kata ya Kiutu, Mheshimiwa Malaki Malambo, ambaye ametoa eneo lenye ukubwa wa mita za  mraba 6,401 na wengine kutoa mita za mraba 5,376.2, eneo ambalo kata hiyo haikuwa nalo.

Hata hivyo wananchi hao, wamesisitiza kuwa wako tayari, kuendelea kujitoa kuchangia nguvu kazi, wakati wote wa utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa shule, huku wakisisitiza kuwa wako tayari kufanya kazi zote za mikono watakazoelekezwa na watalamu wahandisi wa majengo hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, ameungana na wananchi hao katika zoezi la kusafisha eneo hilo, huku akiwapongeza kwa juhudi walizozionesha na kuwataka kuendelea kujitolea katika hauta zote za ujenzi wa shule hiyo mpaka hapo watoto wao, watakapoingia darasani.

Aidha mkurugenzi Msumi, amethibitisha halmashauri kupokea fedha kiasi cha shilingi milioni 470, kutoka Serikali Kuu, kupitia miradi yaake ya SEQUIP, kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Kiutu.

"Serikali imeelekza matumizi ya fedha hizo, shilingi milioni 470, kutumika kujenga jengo la ghorofa litakalobeba  vyumba 8 vya madarasa, Maabara tatu za masomo ya Sayansi,   maabara ya somo la Kompyuta (ICT), Matundu 20 ya vyoo vya wanafunzi pamoja na mfumo wa kuvunia maji ya mvua, wenye matanki mawili ya lita elfu 10 kwa kila moja" amefafanua Mkurugenzi Msumi.

Halmashauri ya Arusha inawashukuru na kuwapongeza wananchi hao, waliokubali kutoa eneo hilo kwa makubaliano ya kufidiwa eneo jingine katika eneo la Gomba Estate lililopo kata ya Mlangarini, kwa pamoja wakiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu, kwa kuwezesha uwepo wa shule ya kata katika kata ya Kiutu kama ilivyo kwa kata nyingine nchini.

ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍✍

PICHA ZA MATUKIO WANANCHI WAKISAFISHA ENEO.


Wananchi wa Kiutu waking'o visiki, kwa lengo la kusafisha eneo tayari kwa kutekelza mradi wa ujenzi wa shule yao ya Kata, shule ya Sekondari Kiutu.


Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameungana na wananchi wa Kiutu, waloojitokeza kusafisha eneo tayari kwa kuanza utekelzaji wa mradi wa kujenga shule ya Sekondari Kiutu, Mkurugenzi huyo akichimba kisiki. 

Wananchi wa Kiutu waking'o visiki, kwa lengo la kusafisha eneo tayari kwa kutekelza mradi wa ujenzi wa shule yao ya Kata, shule ya Sekondari Kiutu.



Wananchi wa Kiutu wakipambana kusafisha eneo, tayari kwa kutekelza mradi wa ujenzi wa shule yao ya Kata, shule ya Sekondari Kiutu.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.