• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAWEZESHAJI MPANGO WA PILI TASAF AWAMU YA TATU WATAKIWA KUWA WAAMINIFU KATIKA KUBAINI KAYA MASIKINI ARUSHA DC

Posted on: August 10th, 2021
  • Na. Eliniap Lupembe.

Wawezeshaji watakaofanya kazi ya kuainisha Kaya masikini 'PAA Facilitator', halmashauri ya Arusha, kupitia mradi wa kipindi cha pili TASAF awamu ya III, wametakiwa kufanyakazi hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa, ili kuwapata walengwa wenye sifa na vigezo  vilivyoaainishwa, kaya ambazo  zinakabiliwa na lindi la   umasikini uliokithiri, ili kufikia malengo ya serikali ya kupambana na adui umasikini kwa maendeelo ya Taifa la Tanzania.

Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, ndugu Seleman Msumi, wakati wa akifungua semina elekezi iliyohusisha wawezeshaji 'PAA', watakaokwenda kuzibaini kaya masikini ambazo zitaingia kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini mpango wa pili wa TASAF awamu ya tatu, pamoja na waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti ya halmashauri hiyo, semina iliyofanyika kwenye viwanja vya halmashauri ya Arusha.

Mkurugenzi Msumi, amewasisitiza kuwa, wawekezaji hao wameaminiwa na serikali  na kuwakabidhi jukumu la kwenda vijijini kubaini kaya masikini zitakazoingizwa kwenye mpango wa ruzuku za TASAF, hivyo wanao wajibu wa katumia fursa vizuri na kwa uadilifu mkubwa, wakiweka uzalendo mbele kwa kufuata vigezo na taratibu zilizowekwa na serikali kupitia TASAF vya kubaini kaya hizo, huku akiwataka waheshimiwa madiwani kutumia majukwaa yao, kuwaeleimisha wanachi sifa na  wajibu wa walengo  katika mradi huo uliotolewa na serikali katika maeneo yao.

"Nina wasihi wawezeshaji wote, tambueni kuwa kazi hii mmepewa ni dhamana ya maisha ya watu, serikali imewaamini, hakikisheni mnaifanya kwa uadilifu na kwa kuzingatia  haki, kila mmoja wenu ahakikishe anabaini na kuandikisha kaya zenye sifa ya umasikini uliokithiri na si vinginevyo, kaya ambazo  zina uhitaji mkubwa wa kusaidiwa na serikali ili waweze kujikwamua, lakini pia waheshimiwa madiwani tambueni mna wajibu wa kuwaelimisha wananchi wenu, kuifahamu vizuri TASAF na mradi huu wa kaya masikini pamoja na wajibu wa walengwa katika mradi huo wa TASAF, tumieni mafunzo haya kuwaelimisha wananchi wenu ili kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima". Amesisitiza Mkurugenzi Msumi.

Aidha, Mkurugenzi Msumi, amefafanua kuwa, lengo la kuendeleza mradi huu ambao tayari, ulifanya vizuri katika awamu ya kwanza, serikali imeona ni vyema kuendelea na mradi huo kwa awamu ya pili, na kuzifikia kaya masikini na zenye sifa katika vijiji vyote vya halamshauri na nchi nzima, lengo likiwa ni kuziwezesha kaya hizo, kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa za kujiongezea kipato, huduma za jamii na kuwekeza katika kuendeleza watoto, pamoja na kuondokana na lindi za umasikini uliokithiri kwa maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa halamshauri ya arusha, mhe. Ojung'u Salekwa, amesema kuwa, zoezi la kubaini kaya masikini, ni zoezi la msingi mno, katika halmashauri ya Arusha, kutokana na ukweli kwamba kaya nyingi hususani kwenye maeneo ya vijijini ziko kayika hali mbaya kiuchumi, zikikabiliwa na changamoto za kuendesha maisha na kushindwa kumudu hata kupata mlo mmoja kwa siku.

"Ninaiponheza serikali ya awamu ya sita, kwa kuona umuhimu wa kuzifikia kaya masikini kwenye vijiji vyote vya halmasha, halia ambayo licha ya kuwezesha kaya hizo kujimudu kiuchumi lakini itapunguza malalamiko yaliyokuwepo kwa serikali, kupitia mafunzo haya, mimi na madiwani wenzangu, tuna jukumu lamkuelimisha wananchi wetu, waufahamu mradi huu wa TASAF, sifa za kaya zinazohitajika pamoja na wajibu wa kaya masikini katika miradi hiyo ya TASAF" Amefafanua Mheshimiwa Ojung'u

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TASAF Makao Makuu, Meneja Miradi ya Ajira za Muda, Ndugu Paul Kijazi, ameweka wazi sifa za walengwa watakoandikishwa katika kipindi cha pili cha mradi wa TASAF awamu ya tatu, ni mpamoja kaya zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi na zenye watoto, kazi zenye watu wenye ulemavu na wagonjwa wa muda mrefu lakini zisizo na watoto, kaya zenye wazee na watoto na kaya zinazoongozwa na watoto.

Aidha Kijazi amefafanua kuwa, licha ya kuwa mradi huu,utatoa ruzuku ya fedha kwa kaya masikini lakini pia kutakuwa na miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa, amabpo kaya itataikiwa kuandikisha watu wawili kufanya ajiro99a za muda,  lengo likiwa ni kuongezea kaya kipato pamoja na kuwaonhezea ujuzi kupitiankazi husika.

Hata hivyo wawekezaji hao 45, wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa umahiri na umakini mkubwa huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa, kupitia  weledi na uzalendo, kwa maendeleo ya kaya masikini ili waweze kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini uliokithiri.

Awali, katika kipindi cha pili cha mradi wa  TASAF awamu ya pili, ulizinduliwa rasmi mwaka 2020 mpaka 2023, na unategemea kutumia kiasi cha shilingi trilioni 2.3 na kutekelezwa katika halmashauri 184 za Tanzanzia Bara na visiwani, na kufika jumla ya kaya milioni milioni moja na laki nne na nusu, zenye jumla ya watu milioni saba kote nchini, huku halmashauri ya Arusha, ukitegemea kutekelezwa katika kata 27 na vijiji 67?

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akizungumza na wawezeshaji wa awamu ya pili ya mradi wa TASAF awamu ya III, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti na wawezeshaji wa mradi, mafunzo yaliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri ya Arusha.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mjeshimiwa aojung'u Salekwa, akizungumza na wawezeshaji wa awamu ya pili ya mradi wa TASAF awamu ya III, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti na wawezeshaji wa mradi, mafunzo yaliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri ya Arusha.


Meneja Miradi ya Ajira za Muda TASAF, Paul Kijazi akizungumza na wawezeshaji wa awamu ya pili ya mradi wa TASAF awamu ya III, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti na wawezeshaji wa mradi, mafunzo yaliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri ya Arusha.



Waheshimiwa Madiwani halmashauri ya Arusha, wakifuatilia mada kuhusu awamu ya pili ya mradi wa TASAF awamu ya III, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti na wawezeshaji wa mradi, mafunzo yaliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri ya Arusha.



Wawezeshaji 'PAA Facilitator', halmashauri ya Arusha, wakifuatilia mada kuhusu awamu ya pili ya mradi wa TASAF awamu ya III, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti na wawezeshaji wa mradi, mafunzo yaliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri ya Arusha.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.