Na. Elinipa Lupembe.
Wazazi na walezi wametakiwa kutimiza majukumu yao, ya kuwahudumia watoto wao hasa watoto wa kike, kwa kuwapungumzia muda wa kufanyakazi za nyumbani pamoja na kuwapatia watoto hao, mahitaji yote muhimu ya shule ili kuwaepusha na viishawishi, wanavyokumbana navyo kutoka kwa wanaume, lengo ni kuwawezesha kujielekeza zaidi kwenye masomo.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimi Msingi, halmashauri ya Arusha, mwalimu Hosein Mghewa, alipokuwa akifungua na kufunga kikao kazi, kilichohususha wadau ya masuala ya kupinga ukatiki dhidi ya watoto wa kike, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mghewa amesema kuwa, watoto wa kike wanakutana na vikwazo vingi sana katika kipindi chao cha masomo, huku wazazi na walezi wakiwa chanzo cha vikwazo hivyo, kwa kutotimiza majuku yao kwa watoto hao, hasa kutowapatia mahitaji yao ya muhimu shuleni.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wazazi na walezi wameshindwa kutekeleza majukumu yao, badala yake, kuwaachia watoto wa kike kufanyakazi za nyumbani kabla na baada ya muda wa shule pamoja kushindwa kuwapa mahitaji yao muhimu ya shule, jambo linalosababisha wasichana kushawishiwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa wanaume, na kujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ngono, na kuweka kando masuala ya shule.
Amewataka wazazi na walezi kutimiza majukumu yao ya malezi kwa watoto wa kike, licha ya kuzungumza na watoto wao na kuwajengea uwezo wa kujiami, lakini pia wanapaswa kuwapunguzia kazi za nyumbani na kuwapatia mahitaji muhimu, jambo amabalo litawaepusha wasichana, kuingia kwenye mitego na vishawishi vya zawadi katoka kwa wanaume.
"Wazazi na walezi msikwepe majukumu yenu, wahudumieni watoto wenu hata kama hali ni ngumu, unakuta mtoto anafanyishwa kazi nyingi asubuhi, anakwenda shule kwa kuchelewa, hana mafuta ya kujipaka, vitaulo vya hedhi, hana kalamu wala daftari, inamlazimu kujitafutia yeye mwenyewe, jambo ambalo ni rahisi kwa mtoto huyu kushindwa kuepuka vishawishi, pindi akutanapo na mwanamme wa kumpatia vifaa hivyo, " amesema Afisa Elimu huyo.
Hata hivyo walimu, walioshiriki kikao kazi hicho, wamekiri baadhi ya wanafunzi kutokuwa na vifaa vyote vya shule, ikionesha dhahiriwazazi kutokwapatia watoto wao, mahitaji muhimu ya shule, huku watoto hao wajihangaikia kupata mahitaji hayo kwa kufanya vibarua au kuomba kwa wenzao.
Aidha walimu hao wamethibitisha kuwepo tofauti kubwa ya kimasomo kati ya mtoto ka kike na wakiume, inayotokana na mila na desturi, huku wakilalamikia wazazi kuwapa kazi nyingi watoto wa kike kabla na baada ya kutoka shuleni, jambo linasababisha wasicha kukosa muda wa kujisomea wawapo nyumbani, tofauti na watoto wa kiume.
Wameongeza kuwa mila na desturi za kabila la kimaasai, mtoto wa kiume akishatahiriwa, haruhusiwi kufanyakazi za nyumbani, hivyo majukumu yote yanamuangukia mtoto wa kike, huku mtoto wa kiume akiwa na muda mwingi wa kujisoma na mtoto wa kike akikosa muda wa kujisomea awapo nyumbani.
Naye mwalimu John Mduma wa shule ya sekondari Ilkiding'a, amethibitsha kuwa, baadhi ya wanafunzi shuleni hapo, hawana vifaa vyote vya shule, na kuthibitisha baadhi ya wazazi kishindwa kitimiza mahitaji muhimu ya mtoto jambo ambalo linasababisha watoto kuingia kufanya vibarua ili wapate mahitaji huku baadhi ya watoto wa kike wakiinhia kwenye vitendo vya ngono.
Ameweka wazi kuwa, endapo wazazi na walezi wataona umuhimu wa kuwapa watoto mahitaji yao muhimu ya shule, watoto watajikita zaidi kwenye masomo na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kingono.
Hata hivyo wanafunzi waliohudhuria kikao kazi hicho, walipata fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili watoto wa kike na kuwaomba walimu kupunguza ukali dhidi ya wasichana, badala yake kuchukua muda kuwasikiliza changamoto zinazowakabili, na kuwasaidia kuzitatua kwa njia sahii, wakiamini kuwa ikiwa nyumbani wazazi wao, hawana uelewa juu ya elimu ya mtoto wa kike, hivyo tegemeo kubwa la watoto hao ni walimu wao.
Wamesema kuwa mila na desturi za kabila lao msichana huchumbiwa akiwa mdogo, mchumba akitaka kumchukua binti wazazi humlazimisha mtoto kuolewa na hata akipata ujauzito wazazi humfundisha mtoto kutokumtaja aliye mpa ujauzito, kitu kinachosababisha wasichana wengi kukatishwa masoma, kupoteza haki na kupoteza ndoto zao.
Awali kikao kazi kazi hicho kimeandaliwa na shirika la CWDC, lengo likiwa ni kutambulisha Mradi wa Kuwajengea Uwezo watoto wa kike kupinga ukatili wa kijinsia katika kata za 7 za Ilkiding'a, Kimnyaki, Bangata, Olkokola, Mwandet, Oloirien na Olturoto katika shule sekondari na msingi zilizopo katika kata hizo.
Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita kianzia sasa, kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Arusha na shirika la CWCD kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society Tanzania.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.