• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI JAFO ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UJENZI ARUSHA DC

Posted on: July 9th, 2020
  • Na. Elinipa Lupembe.

Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo, ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, miradi ambayo inafanyika kwa kiwango cha kuridhisha hasa kwa kuzingatia vigezo vya thamani ya pesa na kukamilika kwa wakati.

Waziri Jafo, ameweka wazi hisia zake, alipotemblea na kukagua mradi wa ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni, kata ya Oljoro na kujionea namna kituo hivyo kilivyojengwa kwa utalamu mkubwa, huku kikiwa tayari kimeanza kufanyakazi ya kuwahudumia wananchi wa kata ya Oljoro na Kata za jirani za mkoa wa Manyara.

Waziri Jafo licha ya kuwapongeza watendaji, kwa kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muri pamoja na watendaji wa halmashauri ya Arusha, amekiri kujivunia sana utekelezaji wa miradi, unaofanyika katika halmashauri hiyo, hasa kwenye ujenzi wa miundombinu katika sekta ya Afya na Elimu, tofauti na halmashauri nyingine nchini.

"Ninafarijika sana kuleta fedha za miradi Arusha DC, kwa kuwa miradi  inafanyika kwa viwango vya hali ya juu, serikali imeleta milioni 500 za kujenga kituo cha Afya Nduruma, mradi ukakamilika vizuri, ikaleta tena milioni 400 za kituo hiki cha Mbuyuni, nacho kimekamilika kwa wakati, majengo yako imara yakionesha wazi  thamani ya pesa iliyotumika" amesema Waziri Jafo.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, licha ya kumshukuru Waziri Jafo na Serikalo ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri iliyotukuka ya usimamizi wa miradi katika halmashauri zote, amemuomba Waziri huyo, kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje 'OPD', hospitali ya wilaya ya Olturumet pamoja na wataalamu katika sekta ya afya ikiwemo, madaktari na wauguzi.

 " Mheshimiwa Waziri, ili kukamilisha mikakati ya Serikali ya awamu ya tano, ya kusogeza huduma za afya kwa wananchi hasa waishio vijijini, na kupata thamani halisi ya majengo yote yaliyojengwa, ninakuomba utuletee watumishi wa sekta ya afya ili wananchi wa Arumeru waweze kutibiwa kwenye majengo haya mazuri" amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, halmashauri ya Arusha imepokea kiasi cha shilingi milioni 900, kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa Kituo cha afya Mbuyuni kwa shilingi milioni 400 na kituo cha Afya Nduruma kwa shilingi milioni 500,  huku upatikanaji wa dawa thelathini muhimu na vifaa tiba ukifikia asilimi 90.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.