• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI KARUKI ABAINISHA VIPAUMBELE SABA VITAKAVYOWEKEWA MKAZO NA TAMISEMI...

Posted on: November 3rd, 2022

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amebainisha vipaumbele na maeneo ambavyo Wizara itawekea mkazo katika kipindi ambacho atakuwa akihudhumu katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Amebainisha hayo leo tarehe 03 Novemba, 2022 wakati alipopewa nafasi na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kutoa salamu kwa Wabunge wakati wa mkutano wa tisa, kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Kairuki amesema atashirikiana na viongozi wa Wizara hiyo kuweka mifumo endelevu ya kitaasisi ambayo itaendelea kudumu hata katika vipindi ambapo viongozi watakapobadilishwa na kuletwa wengine.

Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaweka mkazo wa kudhibiti matumizi mbalimbali fedha za miradi ya maendeleo na matumizi mengineyo katika Halmashauri ili kuhakikisha taratibu za kifedha zinazingatiwa.

Aidha, Waziri Kairuki amesema atasimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha za umma kwa kujiridhisha kuwa matumizi yanayofanyika ni yale yanayohitajika.

Katika ukusanyaji na ukadiriaji mapato, Waziri Kairuki amesema kuna baadhi ya Halmashauri hukadiria viwango vya chini ili kwenye makusanyo waonekane wamevuka lengo, hivyo katika mwaka wa fedha ujao watapitia kila Halmashauri kujiridhisha vyanzo vya mapato na makadirio yao.

Amesema atahakikisha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kukuza mapato katika Halmshauri.

Vile Vile, Waziri Kairuki amesema TAMISEMI itaweka makazo katika usimamizi wa utoaji wa huduma mbalimbali kama afyamsingi, elimu na uboreshaji wa miundombinu barabara kupitia TARURA ili kuboresha maisha ya Watanzania.

Pamoja na mambo Mengine, Wizara itawajengea uwezo wa watumishi ili watekeleze vyema majukumu yao katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kuendeleza kazi ambazo watangulizi walifanya katika Ofisi ya Rais -TAMISEMI.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.