Tatizo la maji kwa wakazi wa halmashauri ya Arusha linategemewa kupungua ifikapo mwaka 2018 kwa kuongeza upatikanaji wa maji hadi kufikia zaidi ya 80% kutoka aslimia 54.2 za sasa.
Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele alipokutana na wataalam wasimamizi wa mradi wa maji wa vijiji vitano halmashauri ya Arusha kwenye hotel ya Mount Meru jijini Arusha na kuthibitisha kuwa mkakati wa serikali ni kuhakikisha maji yanapatikana kwa asilimia 90% .
Waziri Kamwele amethibitisha kutekeleza ahadi yake ya shilingi bilioni 2.3 aliyoitoa mwezi Februari, 2017 ya kupanua mradi wa maji wa OLMULO unaohudumia wakazi wa kata za Oljoro na Laroi halmashauri ya Arusha.
Mheshimiwa Kamwele amesema kuwa fedha hizo zitatolewa ndani ya mwaka huu wa fedha ili huduma ya maji ipatikane umbali usiozidi mita 400 kwa kila mwananchi.
Hata hivyo Waziri Kamwele ameahidi kutoa fedha nyingine kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili kuendeleza chanzo cha maji cha Emutoto kilichogundulika wakati wa upembuzi yakinifu wa mradi wa maji wa vijiji vitano mradi unaotekelezwa na shirika la kimataifa la WaterAid.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.