• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

BENKI YA POSTA YAPANIA KUPANDISHA TAALUMA SEKONDARI NDURUMA

Posted on: October 7th, 2019

Benki ya Posta Tanzania - TPB, imejipanga kupandisha kiwango cha taaluma kwa wasichana wanaosoma, shule ya sekondari Nduruma, halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru.

Mkakati huo umewekwa wazi na Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa matofali 1000 na mifuko 100 ya saruji, vyenye tamani ya shilingi milioni 3.5, kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa  bweni la wasichana, iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Moshingi amesema kuwa, Benki ya Posta Tanzania, imeamua kutoa msaada huo, kwa lengo la kuwanusuru wasichana wa shule ya sekondari Nduruma, kutoka na changamoto wanazokumbana nazo, kuanzia nyumbani mpaka kufika shuleni, zinazochangia kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao, pamoja na kuunga mkono juhudi za wananchi wa Nduruma, ambao tayari wamekamilisha ujenzi wa msingi wa jengo  la bweni hilo.

Ameongeza kuwa, licha ya kuwa watoto wote kuwa na haki sawa, lakini watoto wa kike wapo kwenye hatari kubwa wakiwa njiani kuelekea shuleni, hatari zinayowasababishia  mimba na ndoa za utotoni hadi kufikia kushindwa kuendelea na masomo na  kukatiza ndoto zao.

Aidhaa Moshingi, amefafanua kuwa, Benki ya Posta Tanzania, ni benki ya watanzania hivyo,  hutoa kiasi cha faida inayoipatikana na kuirudusha kwenye jamii, kwa kuchangia miradi mbalimbali kwenye sekta za elimu na afya, sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha miundombinu kwenye sekta hizo, ili wananchi waweze kupata huduma bora zaidi.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari Nduruma mwalimu, Hilda Zoya licha ya kuishukuru Benki hiyo ya Posta, amethibitisha uwepo wa changamoto ya umbali wa maeneo, wanayoishi wanafunzi wa shule hiyo, jambo linalosababisha kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao, huku kiwango cha ufaulu kikiwa ni cha chini.

Ameeleza kuwa, wanafunzi wa shule hiyo, wametoka kwenye jamii ya wafugaji, jamji ambayo wengi huishi mbali kutafuta malisho, na kuwafanya baadhi ya wanafunzi kutembea kati ya Kilomita kumi na kumi na tano, kwenda na kurudi shuleni kila siku, na kuwasababishia uchovu na wengine kushindwa kuhudhuria shuleni kila siku, jambo linaloathiri kwa kiasi kikubwa mchakato mzima wa kufundisha na kujifunza.

"Wanafunzi wakifika shuleni wamechoka na wakati mwingine mahudhurio yao ni ya kususua na kusababisha ufundishaji kuwa mgumu, pamoja na kudumaza taaluma na ufaulu kuwa wa kiwango cha chini" amesema mkuu huyo wa shule.

Hata hivyo wanafunzi wa shule hiyo, wameishukuru benki hiyo, kwa kutambua changamoto yao, na kueleza kuwa uwepo wa mabweni hayo ya wasichana, utaongeza ari ya kusoma na kupenda shule, ari ambayo inatoweshwa na umbali mrefu wanaotembea wakati wa kwenda na kurudi shuleni na kusababisha uchovu na kukata tamaa.

Eliya Obadia, mwanafunzi wa kidato cha tatu, amefafanua kuwa, wasichana ndio wanaoathirika zaidi na changamoto ya umbali huo, hasa wakati wa mvua, hushindwa kuvuka makorongo yaliyojaa maji na kushindwa kuhudhuria shuleni pindi mvua kubwa zikinyesha.

"Wakati wa mvua makorongo hujaa maji, wasichana wanogopa kuvuka, bora sisi wavulana huwa tunajitahidi kupambana kuvuka lakini mara nyingi wasichana wao hushindwa na kulazimika kurudi nyumbani" amethibitisha Eliya.

Mwenyekiti wa Kamati ya shule, Thobias Lonyamali, amewataka wanafunzi hao, kuongeza bidii katika masomo yao na kutambua kuwa, wazazi wao wanajinyima mahitaji mengine na kuamua kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule, ili wao waweze kusoma vizuri kwa mafamikio yao ya baadaye.

Awali ujenzi wa bweni hilo unategemea kugharimu kiasi cha shilingi milioni 56 na mpaka sasa msingi wa bweni hilo, umekamilika kwa kujengwa kwa nguvu za wananchi wa kata ya Nduruma kwa gharama ya shilingi milioni 5.2, huku bweni hilo likitegemewa kulaza jumla ya wanafunzi wakike 70.

Shule ya sekondari Nduruma ina jumla ya wanafunzi 544, ikiwemmo  wavulana 234 na wasichana 310, ikiwa inakabiliwa na changamoto ya wanafunzi kuishi maeneo ya mbali na shule, changamoto inayosababisha wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni.

PICHA ZA MATUKIO:

Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya Posta Tanzania, akimkabidhi mifuko ya saruji, mkuu wa shule ya sekondari Nduruma mwalimu Hilda Zoya.


Afisa Mtendaji Mkuu, Benki ya Posta Tanzania, akikabidhi matofali wa Mkuu wa shule ya sekondari Nduruma, mwl. Hilda Zoya(katikati) na Afisa Elimu Taaluma Idara ya Elimu Sekondari Charles John (wa kwanza kulia)











Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.