HISTORIA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA.
Karibu Halmashauri ya Arusha kufahamu Historia fupi ya Halmashauri hii ikiwemo Halmashauri Chimbuko, ukubwa wa eneo na maeneo ya kiutawala ikiwemo Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji, mipaka yake, Jiografia ya mahali ilipo, Uongozi kiutawala, Idadi ya watu, wenyeji wa halmashauri ya Arusha, shughuli wanazofanya wenyeji. Mahali zilipo Ofisi za Makao Makuu ya halmashauri ya Arusha. Pamoja na Dira, Maono, Malengo na Mikakati ya Halmashauri kwa kipindi cha Miaka Mitano.
MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA:
Ofisi Za Makao Makuu ya Wilaya ya Arusha zipo Kata ya Kiutu Kijiji cha Engorika eneo la Sekei Mkabala na Hoteli ya Kimataifa ya Mount Meru umbali wa takribani mita 300 kutoka barabara kuu ya Moshi – Arusha- Namanga.
CHIMBUKO LA HALMASHAURI YA ARUSHA:
Halmshauri ya Wilaya ya Arusha ilianza rasmi tarehe 01.07.2007 baada ya kugawanywa iliyokuwa Halmashuri ya Meru na kuwa na Halmashauri mbili za Halmashauri ya Meru na Halmashauri ya Arusha.
Halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa Halmashauri saba za mkoa wa Arusha inapatikana chini ya Mlima Meru ikiwa imepakana na halmashauri ya Meru kwa upande wa Mashariki, Halmashauri ya Monduli upande wa Magharibi, Halmashauri ya Longido upande wa Kaskazini Magharibi, Halmashauri ya Simanjiro mkoa wa Manyara kwa upande wa Kusini. Halmashauri ya Arusha imelizunguka jiji la Arusha kwa pande zake zote.
Halmshauri ya Arusha ina eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 1446.692 inapatikana Magharibi mwa mlima Meru wenye urefu wa mita 4,562 kutoka usawa wa bahari ambao ni mlima wa pili kwa urefu Tanzania baada ya mlima Kilimanjaro wenye urefu wa mita 5,890.
Halmashauri ya Arusha imelala kati ya Latitudo 3000- 3040’ Kusini mwa Ikweta na Longitudo 36015’-360 55’ Mashariki.
UKUBWA WA ENEO:
Wilaya ina eneo la kilomita za mraba 1,446.692. Matumizi makubwa ya ardhi katika Wilaya ni pamoja na: kilimo, makazi, biashara, madini, ufugaji / malisho, utalii wa asili na viwanda vidogo na biashara na hifadhi za misitu.
Ambapo, hifadhi ya misitu ina eneo la kilomita za mraba 54.17, ardhi inayofaa kwa kilimo ni Kilomita za mraba 446.56, malisho huchukua eneo la Kilomita za mraba 506.01 sehemu ya ardhi iliyobaki yenye ukubwa wa wastani wa Kilomita za mraba 440.2 inatumika kwa shughuli nyingine kama vile biashara, makazi na madini.
ENEO LA UTAWALA:
Halmashauri ya Arusha ina tarafa tatu za Enaboishu, Moshono na Mukulat ikiwa na kata 27 za Bangata, Bwawani, Ikiding’a, Ilboru, Kimnyaki, Kiranyi, Kisongo, Kiutu, Laroi, Lemanyata, Matevesi, Mlangarini, Mwandet, Moivo, Musa, Nduruma Oldonyosambu, Oldonyowas, Olkokola, Oljoro, Olmotony, Oloirieni, Olturoto, Olturumet, Sambasha, Sokon II na Tarakwa; Ikiwa na Vijiji 67, Vitongoji 256 pamoja na Mamlaka moja ya Mji Mdogo inayojulikana Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni yenye kata 7 na Vitongoji 21.
Halmashauri ya Arusha ina Jimbo Moja la Uchaguzi la Arumeru Magharibi lenye Mbunge mmoja na Madiwani 36 kati ya hao Madiwani 27 ni wa kuchaguliwa na Madiwa 9 wakuteuliwa - Viti Maalum. Halmashauri ya Arusha inaongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye amechaguliwa na Madiwani 36.
HALI YA HEWA:
Halmashauri ya Arusha hii hupata mvua kwa wastani wa mm 500 hadi mm 1200 kwa mwaka. Hali ya hewa ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ina sifa ya misimu miwili ya mvua, mvua za muda mrefu na mvua za vuli. Mvua za muda mrefu huanza mwezi Aprili hadi mwanzoni mwa mwezi Juni wakati mvua za vuli huanza mwezi Oktoba hadi Desemba ambazo ni kati ya mm 800 hadi mm 1000 kwa mwaka. Mvua za wastani kwa mwaka ni mm 900 zikiwa na kiwango cha chini cha unyevu wa asilimia 42 na kiwango cha juu cha unuyevu ni asilimia 50, wakati joto ni kati ya nyuzi 160C hadi nyuzi 330C mwaka mzima. Kasi ya upepo ni kati ya kilomita 6 na 7 kwa saa, hali ya hewa ya baridi hutokea katika miezi ya Juni hadi Agosti joto likiwa ni kati ya nyuzi 160C na 280C.
IDADI YA WATU:
Kutokana na Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 halmashuri ya Arusha ina jumla ya watu 323,198 ikiwa wanaume 154,301 na wanawake 168,897 kwa ukubwa wa
277.4 ikiwa na ongezeko la asilimia 3.4%., Kaya 72,289 ikiwa na wastani wa watu watano kwa kaya.
WENYEJI WA HALMASHAURI YA ARUSHA:
Wenyeji asili wa Halmashauri ya Arusha ni Wamasaai na Wameru na wakazi wengine ni wachaga, wapare, wambulu, warangi, wanyeramba, Wagogo na wasuksuma waliohamia kutoka wilaya za mikoa ya jirani na mkoa wa Arusha kutokana na shughuli za biashara na za kijamii.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI:
Sehemu kubwa ya wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha wanajishughulisha na kilimo na ufugaji, Utalii, Biashara za Makampuni makubwa na madogo, Biashara ndogondogo na wajasiriamali wakubwa na wadogo. Aidha wakazi wengine wana ajira katika: -
Katika uendeshaji wa biashara kuna zaidi ya biashara 1,500 zikiwemo maduka ya rejareja, migahawa, kuendesha nyumba za kulala wageni, machinjio, ususi, uuzaji wa mbao na nguzo, uuzaji wa vifaa vya ujenzi, mashine za kusaga, useremala, ujenzi, kutengeneza vifaa vya chuma n.k. Makampuni makubwa na madogo yanayojishughulisha na utalii (cultural tourism), ikiwa ni pamoja na uwindaji. Wakulima wadogowadogo wanaojishughulisha zaidi na kilimo cha mboga mboga na kukuza miche ya miti.
UONGOZI:
HISTORIA YA WENYEVITI HALMASHAURI YA ARUSHA TANGU KUANZISHWA KWAKE MWAKA 2007:
Na.
|
Jina Kamili
|
Mwaka alioanza
|
Mwaka alioondoka
|
1.
|
Mhe. John Ole Saitabau
|
2007
|
2010
|
2.
|
Mhe. Simon Ole Saning’o
|
2010
|
2015
|
3.
|
Mhe. Noah L. Saputu
|
2015 | 2020 |
5. | Mhe. Ojungu P. Salekwa | 2020 | 2025 |
HISTORIA YA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA TANGU KUANZISHWA KWAKE MWAKA 2007:
Na.
|
Jina Kamili
|
Mwaka alioanza
|
Mwaka alioondoka
|
1.
|
Halfan H. Hida
|
Julai 2007
|
Februari 2013
|
2.
|
Fidelis S. Lumato
|
Februari 2013
|
Aprili 2016
|
3.
|
Dkt. Wilson M. Charles
|
Julai 2016
|
Oktoba 2019 |
4. | Alvera Ndabagoye | Oktoba 2019 | Julai 2020 |
5. | Saad Mtambule | Julai 2020 | Juni 2021 |
6. | Seleman Msumi | Julai 2021 | - |
Julai Mosi 2017, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha iliadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake kutokana na kugawanywa kwa Halmashauri ya Wilaya ya zamani ya Arumeru.
Mwaka 2017 halmashauri ya Arusha imeandaa Mpango Mkakati wa mika miatano kwa mwaka 2016/2017 - 2020/2021, kwa mujibu wa matakwa ya
Sheria Namba 9 ya mwaka 1982 ambayo inahitaji Serikali za Mitaa (Halmashauri) kuandaa Mipango Mikakati ya miaka mitano ili iweze kutumika kama miongozo wakati wa maandalizi yaa Mpango wa Muda wa Kati na Muundo wa Bajeti ya Matumizi (MTEF).
Mpango Mkakati ulianisha vipaumbele katika utoaji wa huduma na utaratibu wa kawaida wa mapitio ya kila mwaka uliofanywa na jamii.
Mpango Mkakati huu wa miaka mitano (2016/2017 - 2020/2021) una lengo la kukamilisha Dira ya Halmashauri ya Wilaya ya kuwa kuongoza Halmashauri iliyobadilishwa inayotoa huduma zenye ubora wa juu kwa ajili ya maendeleo endelevu ya jamii ifikapo mwaka 2025.
Mpango mkakati huu wa 2016 / 2017 - 202/2021 unasisitiza katika kuboresha utoaji huduma kwa jamii ya Wilaya ya Arusha kupitia matumizi sahihi na yenye ufanisi ya rasilimali.
MAONO:
Kubadili Jamii kwa kutoa huduma bora na kuleta maendeleo endelevu kwa Jamii ifikapo 2025.
DIRA:
Kutoa huduma bora kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi ili kuleta tija na maendeleo endelevu kwa Jamii.
MALENGO MAHUSUSI:
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.