Na. Elinipa Lupembe.
Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Arusha, imejipanga vema kushiriki katika kutekeleza mradi wa TCI -Tupange Pamoja, kwa kuhamasisha umma kupata elimu ya afya ya uzazi kwa vijana, kupitia mpango wa Huduma Rafiki kwa Vijana kupitia makundi maalumu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, amesema kuwa, idara yake inashughulika na makundi mbalimbali ya jamii, ameahidi kutumia fursa hiyo kuhamasisha umma, kutekeleza mradi huo wa Tupange Pamoja na Tuwaveshe Salama, mradi unaotekeleza na halmshauri kwa ufadhili wa shirika la JPEIGHO.
Angela amethibitisha, kutumia fursa ya majukwaa hayo, kutoa elimu na kuwahamasisha juu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana pamoja na Upatikanaji wa Huduma rafiki kwa vijana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
"Tunakutana na makundi ya Wanawake, Vijana na walemavu kwa ajili ya kutoa elimu ya ujasiriamali na mikopo, tunakunata na makundi ya watoto na vijana wanaoishi kwebpnye mazingira magumu, na pia tuna klabu za watoto shule za msingi na sekondari, kupitia makundi haya elimu ya Afya ya uzazi kwa vijana itafika kwa watu wengi zaidi" amesema Afisa huyo.
Aidha amefafanua kuwa, taarifa hizi zikiifikia jamii kwa usahihi kupitia makundi mbalimbali, ni rahisi kuokoa vijana wengi kuingia kwenye ndoa za utotoni, ndoa na watoto wasiotarajiwa na kuwafanya vijana kujitambua na kutimiza ndoto zao na kuwa na taifa bora lenye watu wenye afya bora.
Hata hivyo Angela amefafanua zaidi kuwa, mtazamo hasi wa jamii yetu, juu ya Afya ya uzazi kwa vijana, unaofanya jamii hasa wazazi kudhani mtoto akijifunza mambo ya uzazi atajiingiza kwenye kwenye vitendo vya ngono.
Ameitaka jamii kuachana na mawazo hayo potofu na kutambua kuwa elimu ya afya ya uzazi ina lengo la kumfanya kijana kutambua mabadiliko ya mwili wake, athari na madhara ya mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana na mihemko ya mwili wake, namna ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na kujamiiana na jinsi ya kujikinga.
Hata hivyo imefahamika, vijana hawana taarifa sahihi juu ya afya ya uzazi, badala yake hufundishana wao kwa wao na matokeo yake, hujikuta kuanza kujamiiana na kujikuta, wakilazimika kuingia kwenye ndoa za utotoni kutokana na mimba zisizotarajiwa, umefika wakati sasa kuwawezesha vijana kupata taarifa sahihi, juu ya afya zao ili kujipanga na kujiandaa na maisha yao ya familia ya baadaye bila kuathiri masomo na mipango ya maendeleo yao.
Huduma Rafiki kwa Vijana, hutoa elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana, na inapatikana kenye vituo vya Afya 15 ndani ya halmashauri ya Arusha, kupitia mradi wa TCI- TUPANGE PAMOJA, mradi uliofadhiliwa na shirika la JHPEIGO.
Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa akizungumza na Mratibu wa Mradi TCI- TUPANGE PAMOJA, Waziri Njau, namna idara yake itakavyotekeleza mradi wa TCI- TUPANGE PAMOJA na HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA.
Afisa M/Jamii, halmashauri ya Arusha akijiunga na kupakua vitini vya masomo TCI-TUPANGE PAMOJA kwenye mtandao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.