Na. Elinipa Lupembe
JE UNAFAHAMU KIBALI CHA UJENZI?
Kibali cha ujenzi ni Moja ya kanuni muhimu sana ya upangaji wa miji nchini Tanzania. Kila anayetaka kujenga nyumba anapaswa kufuata kanuni za ujenzi katika kibali cha ujenzi atakachopewa, mara nyingi kwa mujibu wa Sheria kibali cha ujenzi hutolewa na Mamlaka za Serikali ambazo ni halmashauri kupitia Idara ya Ardhi na Mipango Miji, Idara ya Ujenzi na Idara ya Mazingira.
UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI.
Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi holela mijini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.
UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
•Kutimiza matakwa ya kanuni za ujenzi mijini•Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji ya sehemu husika•Kudhibiti ujenzi holela
TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI.
Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao
•Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector)
Afisa Ardhi (Land Officer)
*Mpima (Land Surveyor)•Afisa Mipango Miji (Town Planning Officer)
•Afisa Afya (Health and Sanitation Officer)Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “Architectural & Structural Drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo.
Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector) – kuona kama michoro inakidhi haja ya kiufundi na specifications.Afisa Ardhi (Land Officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.Mpima wa Jiji (Land Surveyor) – kutambua mipaka halali
Afisa Mipango Miji wa Jiji (Town Planning Officer) – Kuona kama ujenzi unaoombewa ni sahihi kwa mujibu wa michoro ya mipango miji.
Afisa Afya (Health and Sanitation Officer) – kuona kama usafi kwa ujumla na maji taka yatatunzwa vyemaKama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ya mipango miji na utoaji vibali vya ujenzi.
Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya Halmashauri atakayopewa.Mwombaji ataandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na Mhandisi wa Ujenzi na Afisa Mipango Miji wa Halmashauri.
MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI
*Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili (2) hadi manne (4)•Hii ni pamoja na uwasilishaji wa ramani zilizoidhinishwa na wataalamu husika na hati za umiliki zilizo sahihi.
WAJIBU WA MWANANCHI
•Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya mji/jiji kwa kibali kutoka Halmashauri.
TAHADHARI.
•Endapo mwananchi yeyote atajenga nyumba bila ya kupata kibali cha ujenzi toka Halmashauri, atapewa HATI ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku saba (7)
•Kama mwombaji atakaidi AMRI ya kusimamisha, jiji au mji litampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyewe na akishindwa jiji litabomoa jengo husika na kudai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomoaji.
KABLA YA KUQNZA UJENZI, FIKA OFISI ZA HALAMSHAURI YA ARUSHA ENEO LA SEKEI KUPATA KIBALA CHA UJENZI.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.