Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi wa Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta kwa wingi Duniani (Opec Fund), Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF, kadhalika amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha, miradi yote iliyofadhiliwa na OPEC FUND, inakamilika kwa wakati na kuleta matokeo chanya kwa jamii
Hayo aliyasema leo, wakati akikagua miradi ya maendeleo ya inayotekelezwa na TASAF awamu ya III na ya IV, katika shule ya sekondari Oldonyowas, halmashauri ya Arusha, wilaya ni Arumeru, mkoa wa Arusha.
"Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kushirikiana nasi, kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya kuondoa umasikini katika sekta ya elimu na afya, nimefurahi kuona watoto wanasoma katika mazingira bora kwenye madarasa mazuri na mabweni mazuri, shule ina jengo zuri la utawala pamoja na nyumba nzuri za walimu" amesistiza Dkt. Alkhalifa
Aidha, Dkt. Alkhalifa ameongeza kuwa, malengo ya serikali kuanzia mwaka 2020 -2025, ni kuhakikisha inapeleka maendeleo kwa kasi kwa wananchi lengo likiwa ni kukabiliana na wimbi la umasiki, kwa kuwezesha huduma za afya na elimu pamoja na kuwawezesha wananchi kukuza pato la familia kwa maendeleo ya jamii nzima.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF TANZANIA, Ladislaus Mwamanga, amesema kuwa, ugeni kutoka OPEC FUND, umekuja kwa ajili ya kufanya mapitio ya kawaida pamoja na kufanya tathimini ya miradi iliyotekekelezwa na fedha kutoa OPEC FUND.
"Umoja huo unashirikiana serikali ya Tanzania kuchangia miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa ajili ya kupunguza wimbi la umasikini katika jamii, hivyo wamekuja kuona miradi hiyo, kwa ujumla wake na wameona utekelezaji wa miradi na kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu ambayo inawasaidia sana wanafunzi, kwa kuwa wanapata huduma zote za msingi shuleni" amesema Mkurugenzi Mwamanga.
Mkurugenzi Mwamanga, amefafanua kuwa, viongozi wa OPEC walipokutana na Mheshimwa Rais Samia Suluhu Hassan, walitoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 50 sawa na shilingi bilioni 120, kwa ajili ya kuendleza mradi wa kupunguza umasikini awamu ya nne, mradi ambao unatekelezwa katika mikoa mitano ya Tanzania Bara, ambayo ni Arusha Njombe, Simiyu, Mwanza na Geita.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldonyowas, Mhe. Godfray Ayo, ameushukuru Umoja wa nchi hizo zinazozalisha mafuta kwa wingi, kupitia TASAF, kwa kutoa fedha, ambazo zimewezesha ujenzi wa miundombinu ya shule ya sekondari Oldonyowas, pamoja na fedha za kupunguza umaskini kwa wananchi wa eneo hilo, huku akiweka wazi kuwa kijiji cha Oldonyowas pekee kimepata jumala ya shilingi milioni 747.7.
"Wananchi wamenufaika sana na miradi inayotekelezwa na TASAF, kwaa kuwa hali ya umaskini uliokithiri, imeaanza kupungua na kujidhihirisha katika kijiji chetu, watoto wetu wanaendelea na masomo ya sekondari, wananchi wanafanya ufugaji wa biashara kupitia mradi wa ufuaga kuku chotara, wapo wananchi wanaonufaika na mpango wa kuhawilisha fedha, umasikini unaondoaka Oldonyowas" amesisitiza Mwenywkiti huyo
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa kijiji, ameweka wazi kuwa, kijiji cha Oldonyowas pekee kimetekeleza jumla ya miradi sita yenye thamani ya shilingi milioni 747.7, na kufafanua kuwa shilingi milioni 34 zimetekelza mradi wa ufugaji kuku chotara, ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo ulioghatimu shilingi milioni 97.8, milioni 76.7 ujenzi wa nyumba za walimu, milioni 104 ujenzi wa jengo la Utawala, ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana milioni 175.1, na ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana utakaoghatimu shilingi milioni 338.7 Kwa TASAFU awmu ya IV.
ARUSHA DC
KaziIendelee✍✍✍
Mkurugenzi wa OPEC FUND, Dkt. Abdulhamid Khalifa, akiwa na Makamu Mwenyekiti, halmashauri ya Arusha, Mhe. Freddy Lukumai, mbele ya moja ya nyumba za walimu zilizojengwa kwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC FUND, shule ya sekondari Oldonyowas
Mkurugenzi wa OPEC FUND, Dkt. Abdulhamid Khalifa, akikagua moja ya majengo ya nyumba za walimu zilizojengwa kwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC FUND, shule ya sekondari Oldonyowas
Mkurugenzi wa OPEC FUND, Dkt. Abdulhamid Khalifa, akikagua Bweni la wasichana, lililojengwa kwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC FUND, shule ya sekondari Oldonyowas.
Mkurugenzi wa OPEC FUND, Dkt. Abdulhamid Khalifa, akiotesha mti mbele ya Bweni la wasichana, lililojengwa kwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC FUND, shule ya sekondari Oldonyowas.
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi wa OPEC FUND, Dkt. Abdulhamid Khalifa, walimu, wanafunzi na wananchi, wakiwa mbele ya Jengo la Utawala, lililojengwa kwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC FUND, shule ya sekondari Oldonyowas.
Mkurugenzi wa OPEC FUND, Dkt. Abdulhamid Khalifa, akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Oldonyowas.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.