• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TASAF YAWEZESHA UJENZI WA KIVUKO MOIVO, HUKU KAYA ZILIZO KWENYE MPANGO ZIKINUFAIKA NA AJIRA ZA MUDA.

Posted on: June 18th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kupitia mradi wa mpango wa kunusuru kaya Masikini, unaendelea kuzinufaisha kaya hizo, kwa kutoa ajira za muda kupitia miradi iliyoibiliwa na kaya hizo na kutekelezwa katika maeneo yao.

Kijiji cha Moivo, kata ya Moivo ni miongoni mwa vijiji 88 vya halmasahauri ya Arusha, vinavyonufaika na mpango huo unaotekelezwa na TASAF awamu ya III, kikiwa na walengwa 250.

Akizungumza kwenye eneo la ujenzi wa kivuko hicho, mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi Brazard Mkwizu, amesema kuwa mradi wa ujenzi wa kivuko uliibuliwa na walengwa hao, kutokana na adha kubwa waliyokuwa wakiipata wananchi wa eneo hilo kwa kukosekana kivuko, na kuwasilishwa halmashauri, hatimaye TASAF.

Mkwizu ameweka wazi kuwa eneo hilo lilikiwa ni eneo hatarishi kwa wananchi wa Moivo, nyakati zote za mwaka, huku wahalifu wakitumia eneo hilo kukaba na kunyang'anya watu mali zai, wengine kubakwa huku wengine wakinusurika kuuwawa.

Hata hivyo wanufaika  hao wamethibitisha kuwa licha ya TASAF kutatua changamoto ya kivuko katika eneo lao, lakini walengwa hao wamekuwa wakifanya kazi za muda na kulipwa ujira, pesa ambayo huwasaidia kujikimu kimaisha.

"Tunaishukuru serikali kwa kutujengea kivuko, kwa kuwa eneo hili lilikiwa ni hatari hasa nyakati za usiku na alfajiri, vibaka waligeuza kichaka cha wanyang'anyi, tunategemea tatizo hili litakwisha, lakini zaidi sisi walengwa tumepata ajira za muda licha ya kuwa pesa si nyingi sana ila sio sawa na kukosa kabisa, tunafanya kazi kwa moyo kwa kuwa kivuko hiki, kitatusaidia wakazi wote wa Moivo". Amesema Tatu Hamisi mnufaika wa mpango wa Kunusuru kaya Masikini

Naye mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewataka wananchi hao kujitoa kwa moyo wakati wote wa ujenzi mpaka kukamilika kwa kivuko hicho, na akiwasisitiza kukitunza mara baada ya kukamilika.

"Mnapaswa kutambua namna serikali inawathamini na kutatua kero iliyokuwa inawkabili, rai yangu ni kutunza miundo mbinu ya kivuko hiki kwa kiwa serikali intumia fedha nyingi katika kutekeleza miradi, wananchi mnapaswa kuithamini miradi yote" amesisitiza Msumi.

Awali TASAF imetoa kiasi cha shilingi milioni 76 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kivuko, huku shilingi milioni 38 zikitumika katika ujenzi na milioni 38 zikitumika kulipa ujira kwa wanakaya walio kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji hicho cha Moivo,  kwa kufanya kazi za muda kwa masaa na kwa zamu kila siku. 

ARUSHA DC

KaziIendelee✍✍

PICHA ZA WANUFAIKA WAKIFANYA KAZI WAKATI WA UJENZI WA KIVUKO MOIVO.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.