Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha anawatangazia wananchi wote kuwa, halmashauri kwa kushirikiana na Kampuni ya Redding Enterprises Limited, wanauza viwanja 383 vyenye ujazo mbalimbali katika eneo la Mlangarini.
Viwanja vipo umbali wa Mita 700 kutoka barabara ya mpya ya mzunguko 'Ring Road' maarufu kama barabara ya Afrika Mashariki.
Viwanja viko eneo ambalo linafikika kwa urahisi na huduma muhimu za maji, barabara na umeme zinapatikana.
Viwanja hivyo vinauzwa kwa bei ya shilingi elfu kumi na mbili - 12,000/= kwa kila Mita moja ya mraba.
Mwenye nia ya kununua Kiwanja afike kwenye Ofisi ya Ardhi Halmashauri ya Arusha, chumba namba 28.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.