Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bi. Beatrice Barnaba, amesema kuwa ufuatiliaji na usimamizi wa haki za mtoto ni jukumu la kila mmoja katika jamii, na si jukumu la serikali pekee.
Akizungumza katika kipindi cha The Tanzania Leo kinachorushwa na kituo cha Redio Enaboishu FM 101.3, kinachoendeshwa na @geofreyjulius0 Geoffrey Julius, Bi. Beatrice Barnaba alisisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana katika kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vyote vya ukiukwaji wa haki zao.
“Mtoto ni sehemu muhimu ya familia na taifa kwa ujumla. Kumlinda mtoto ni jukumu letu sote kama jamii. Tunapaswa kuhakikisha wanapata malezi bora, elimu, matunzo na ulinzi dhidi ya vitendo vya unyanyasaji,” alisema.
Aidha, alitoa wito kwa wazazi, walezi na viongozi wa mitaa kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa ustawi wa jamii ili kuhakikisha kila mtoto analelewa katika mazingira salama na yenye maadili.
Kipindi hicho kililenga kuelimisha jamii kuhusu nafasi ya kila mtu katika kulinda na kutetea haki za watoto, sambamba na kuongeza uelewa juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na vitendo vingine vinavyohatarisha ustawi wa mtoto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.