MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022
Halmashauri ya Arusha inategemea kufanya Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani (Full Council) wa robo ya tatu mwaka wa fedha 2021/2022, kwa kipindi cha kuanzia Januari mpaka Machi 2022.
Mkutano huo utakaofanyika tarehe 09.05.2022 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:00 asubuhi. Mkutano huo wa baraza la Madiwani utakuwa na ajenda 12, huku agenda kuu zikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, taarifa ya Mapato na Matumizi ya mwezi Machi 2022, Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya robo ya tatu, taarifa ya kuanza utekelezaji wa zoezi la utambuzi, Usajili na ufuatiliaji wa Mifugo pamoja na kujadili Masuala ya Kiutumishi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa. Mkutano Baraza la Madiwani ni Mkutano wa wazi, hivyo wananchi wote wa Halmashauri ya Arusha wanatakiwa kuhudhuria, ili kufuatilia kwa uwazi shughuli za utekelezaji wa Maendeleo zilizotekelezwa katika Halmashauri yao kwa kipindi cha miezi mitatu na robo ya tatu, mwaka wa fedha 2021/2022.
Imetolewa na:-
ELINIPA J. LUPEMBE
AFISA HABARI
HALMASHAURI YA ARUSHA.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.