• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MUDA, JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

Friday 9th, May 2025
@ARUSHA DC

Kiambatisho Na.1


TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

OFISI YA AFISA MWANDIKISHAJI WA JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

HALMASHAURI YA ARUSHA

S.L.P. 2330,

ARUSHA

02/07/2019

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA

Kwa mujibu wa Kifungu cha 7A (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 10 (6) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2018 na Kanuni ya 12 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2018.

Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Arumeru Magharibi anapenda kuwajulisha kuwa, zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata zote za Halmashauri ya Arusha linaanza hivi karibuni. Katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la  Wapiga kura Vituoni, watatumika Waandishi Wasaidizi na BVR Kit Opeators. Hivyo anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hizo;

  • Sifa za Mwombaji wa nafasi ya Mwandishi Msaidizi au BVR Kit Operator
  • Awe raia wa Tanzania.
  • Awe mkazi wa kawaida wa Kata husika anayoombea.
  • Awe na umri usiopungua miaka 18.
  • Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha Nne na ajue kusoma na kuandika.
  • Awe na umahiri katika matumizi ya Kompyuta.
  • Asiwe kiongozi au kada wa Chama cha Siasa.
  • Awe mwadilifu na mwaminifu.
  • Waombaji waliowahi kufanya kazi kiustadi katika zoezi la Uandikishaji mwaka 2015 na wanazo sifa zilizotajwa hapo juu watapewa kipaumbele.
  • Majukumu ya Mwandishi Msaidizi na BVR Kit Operator
  • Kuhakikisha kuwa kituo kinafunguliwa kwa wakati na kuanza uandikishaji kwa muda uliopangwa ambao kwa mujibu wa maelekezo ya Tume ni saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
  • Kubandika bango la Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura na mabango mengine yaliyotolewa na Tume kwa ajili ya kituo cha uandikishaji.
  • Kuhakikisha vifaa muhimu vya kituo vinakuwepo katika Kituo cha kuandikisha Wapiga Kura.
  • Kuwepo kituoni muda wote wa kazi hata kama hakuna Wapiga Kura wanaokuja kujiandikisha au kuboresha taarifa zao.
  • Kusimamia ujazaji wa fomu za Mwombaji (Mpiga Kura) ili kuepusha makosa.
  • Kuingiza taarifa za Mpiga Kura kwenye Mfumo wa Uandikishaji.
  • Kuhakikisha kuwa Wapiga Kura waliokuja kituoni kabla ya saa 12:00 jioni na kupanga foleni wanaandikishwa wote isipokuwa kama wapo wengi, wataorodheshwa majina na kuwapanga kuanza nao siku inayofuata.
  • Kuhakikisha kuwa baada ya uandikishaji wa siku kukamilika, taarifa ya Wapiga Kura walioandikishwa kwa siku hiyo inaandaliwa  na kutunzwa kwa lengo la kumkabidhi Afisa Mwandikishaji Msaidizi ngazi ya Kata.
  • Kuhakikisha kuwa vifaa na nyaraka za uandikishaji vinatunzwa vizuri kipindi chote cha zoezi na kuvikabidhi kwa Afisa Mwandikishaji vikiwa katika ubora wake.
  • Majukumu mengine atakayopangiwa na Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi.
  • Mambo ya kuzingatia wakati wa kutuma maombi
  • Mwombaji lazima aainishe kazi anayoomba kati ya Mwandishi Msaidizi au BVR Kit Operator
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) wawili pamoja na picha 3 (Passport Size) za hivi karibuni.
  • Maombi yote yatapaswa kuambatana na nakala za vyeti vya kitaaluma na kitaalamu.
  • Mwombaji ambaye ni Mtumishi wa Umma atapaswa kupitisha maombi kwa mwajiri wake. Mwombaji ambae si  mtumishi wa Umma, maombi yake yapitie kwa Mtendaji wa Kata wa Kata husika anayoomba kufanya kazi.
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 09/07/2019 SAA 09:30 ALASIRI
  • Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  • AFISA MWANDIKISHAJI
  • JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI
  • SLP 2330

          ARUSHA

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA

WILSON MAHERA CHARLES

AFISA MWANDIKISHAJI

JIMBO LA ARUMERU M

Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.