MAMBO MUHIMU – PIKIPIKI
Ili kupata Leseni ya Pikipiki fika Ofisi za Biashara Ukiwa na viamabatanisho vifuatavyo:-
i.Cheti halisi na kivuli cha usajili wa Pikipiki husika
ii.Bima ya Pikipiki husika
iii.Taarifa ya ukaguzi wa chombo kutoka Kikosi cha usalama barabarani
iv.Leseni halisi ya udereva ,kivuli chake na Picha ya Mmiliki au Dereva
v.Nakala ya Mkataba wa ajira kati ya Mmiliki na Dereva
vi.Eneo mwombaji atakalofanyia biashara hii
(Sehemu ya II Kifungu cha 5)
Masharti ya Kupata Leseni ya Pikipiki:-
1.Mwombaji awe na umri wa miaka 18 na kuendelea
2.Malipo yote yatafanyika Benki ya NMB akaunti ya SUMATRA Na. 20106600550
3.Maombi ya Leseni hufanyika kila Mwezi Juni na Leseni hutolewa mwezi Julai (Mwombaji atakayechelewa kuleta maombi atalipa faini ya 50% ya ada ya leseni yake)
4.Endapo mwombaji atakataliwa atapewa taarifa ndani ya siku 7 tangu siku aliyokataliwa na sababu za kukataliwa.
MASHARTI YA LESENI YA USAFIRISHAJI:-
1.Pikipiki husika lazima ikidhi viwango vya TBS na iwe na mapigo manne
2.Dereva haruhusiwi kubeba zaidi ya abiria mmoja (Mshikaki ni marufuku).
3.Dereva na abiria wavae kofia ngumu kujiepusha na madhara ya ajali wakati inapotokea
4.Dereva anapaswa kuwa msafi na unifomu ya nguo zake kuwa safi na kuwa na namba inayoonekana na kila mmoja kwenye unifomu yake.
5.Dereva huruhusiwi kutumia simu wakati unaendesha
6.Dereva asiendeshe chombo kwa mwendo kasi zaidi ya ulioruhusiwa na bila kuzingatia hali ya barabara pamoja na sheria za usalama zilizomo barabarani.
7.Endapo mmiliki siyo dereva anaweza kuingia mkataba na dereva mzoevu na aliyetimiza masharti ya sheria kukiendesha chombo husika
8.Pikipiki zote za kukodishwa zinapaswa kuwa na Pleti namba nyeupe na maandishi meusi.
9.Pikipiki ifanye biashara kwenye eneo lililoainishwa kwenye leseni na Halmashauri.
10. Dereva huruhusiwi kumpakia mtoto wa chini ya miaka 8 bila kuwa na mtu mzima aliyeongozana naye
ADA ZA LESENI PIKIPIKI ZA MIGUU MIWILI KWA MWAKA
1.Ada Ya Leseni 20,000/=
2.Ada Ya Maombi 2,000/=
----------------------------------
JUMLA 22,000/=
====================================
ADA LESENI PIKIPIKI ZA MIGUU MITATU KWA MWAKA
1.Ada Ya Leseni 30,000/=
2.Ada Ya Maombi 2,000/=
----------------------------------
JUMLA32,000/=
===================================
•ADA KWA AJILI YA NAKALA ILIYOPOTEA AU KUCHAKAA/KUHARIBIKA NI SHILINGI 5,000 TU
Kinabo Liberty Daniel
AFISA BIASHARA MWANDAMIZI NA
AFISA MTEULE PIKIPIKI ZA MIGUU MIWILI NA MITATU
HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.