AFISA UTAMADUNI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA AONGOZA MAZOEZI YA VIKUNDI VYA UTAMADUNI KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bi. Suzana Salvatory, ameendelea kuimarisha maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kushiriki mazoezi na vikundi mbalimbali vya utamaduni kutoka jamii ya Wamasai ndani ya Halmashauri ya Arusha.
Akizungumza wakati wa mazoezi, Bi. Suzana amesisitiza umuhimu wa tamaduni za jamii kuenziwa, akibainisha kuwa sanaa na utamaduni vina nafasi kubwa katika kukuza mshikamano katika kijamii.
Maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani yatafanyika tarehe 08/03/2025 Mkoani Arusha na yanatarajiwa kuhudhuriwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.