Na.Elinipa Lupembe.
# Amewaagiza viongozi wa kata na vijiji kujenga tabia ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi, kwa kupanga kila siku moja katika wiki, na kuitaja siku ya Jumanne kiwa ni siku ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitatua na kuzifikisha sehemu husika kwa wakati, kama ni ofisi ya Mkurugenzi ama ofisi ya mkuu wa wilaya.
# Amewataka viongozi na wanachi kushirikiana kulinda usalama katika eneo lao, na kutoa onya kwa wananchi ambao ni wavunjifu wa amani na usalama, na kuwataka viongozi kuwachukulie hatua za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamni, kwani amani na utulivu ni chanzo cha maendeleo kataka maeneo yetu.
# Amewahimiza wananchi kujituma katika kufanya kazi, na kutambua kuwa kazi ndio msingi wa mendeleo, kila mmoja awe na shughuli halali ya kufanya ya kumuingizia kipato, kwa kufanya kazi kwa bidii, kutawaletea maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.
# Serikali ya awamu ya sita imejielekeza katika kutatua kero za wananchi kwa kusogeza huduma karibu na wananchi, kwa kuhakikisha kila mwananchi anafaidika na huduma zinazotolewa na serikali kisekta.
**** Katika sekta ya Umeme, serikali imepunguza gharama za kuunganisha umeme majumbani hadi kufikia shilingi elfu 27, gharama ambazo kila mwamnanchi anaweza kuzimudu.
**** Serikali imetenga takribani shilingi bilioni 2.5, kwa ajili ya kufanya matengenezo ya barabara, hivyo wanachi wana jukumu la kuzitunza barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
***** Kiasi cha shilingi bilioni 5 kimetengwa kwa ajaili ya kutekeleza miradi ya maji, ikiwa na lengo la kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha kila kaya inachota maji katika umbali usiozidi Mita 400 huku ikienda sambamba na kampeni ya mtue mama ndoo.
*****Katika kupambana na umasikini uliokithiri nchini, serikali imeanza kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa mpango kwa kunusuru kaya masiki kupitia mradi wa TASAF awamu ya tatu, ambapo vijiji vyote nchini vitaingzwa kwenye mpango, huku halmashauri ya Arusha ikiongezewa jumla ya vijiji 43 kati ya vijiji 45 ambavyo vilikuwa kwenye mpango tangu mwaka 2013 idadi ambayo itakamilisha vijiji vyote 88 vya halmashauri.
******Aidha amewataka wazazi kuweka mipango thabiti ya hakikisha wanatimiza majukumu yao, kwa kuwawezesha watoto wao kupata chakula cha mchana wawapo shuleni kwa shule zote za kutwa, huku akifafanua kuwa ili mtoto afanye vizuri katika masomo ni lazima awe na afya bora, afya inayotokana na lishe bora.
ARUEMEU YETU
KAZI IENDELEE✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.