#Ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha 'AUWASA', kuhakikisha Wananchi wanaoishi katika vyanzo vya maji na ambao miundombinu ya mradi huo mkubwa wa maji itawapita kwenye maeneo yao wapatiwe maji, Magufuli.
#AUWASA kuhakikisha mradi huo wa maji unawafikia Wananchi wa kata ya Oldonyosambu, halmashauri ya Arusha Wilayani Arumeru, eneo ambalo lina tatizo la madini ya floraidi iliyozidi inayowaathiri wananchi hao kiafya.
# Amewataka wananchi wote kutunza vyanzo vya maji kwa manipufaa yao na vizazi vijavyo, pamoja kuvithamini huku wakitambua kuwa ' Maji ni Uhai'.
# Wananchi kuithamini na kuitunza miradi inayotekelezwa na Serikali kwa kuwa inatumia fedha nyingi ambazo ni za mkopo wa riba nafuu kutoka Benk ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), na kutambua kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kulilipa fedha hizo, kupitia ulipaji kodi.
# Amewataka Watanzania kuacha tabia ya kukwepa kulipa kodi, kwani kodi wanayoilipa ndio hutumika kutekeleza miradi yote ya maendeleo, na kutambua juwa kodi hiy ni kwa ajili ya maendeleo yao na nchi kwa ujumla.
#Amewaonya baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kulipa kodi kwa kuwapa wamachinga bidhaa zao wawauzie, na kuwataka Wamachinga kutotumika kukwepa kodi kwani wanaikosesha nchi yao mapato.
#Amewaonya pia baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu , na kutoa risiti za TRA 'feki' zenye kuonesha, kiwango kidogo cha fedha tofauti na kiwango cha fedha iliyotolewa na mteja.
#Ameitaka TRA kuacha kuwakadiria viwango vikubwa vya kodi ambavyo kiuhalisia, wafanyabiashara wanashindwa kulipa na kuwata kuweka viwango vya kodi ambavyo vinalipika huku akiwasisitiza TRA kufanya utafiti wa kwanini wananchi wanakwepa kulipa kodi.
# Ameipandisha hadhi barabara yenye urefu wa Kilomita 18, kutoka Mianzini kupitia Ilikidinga hadi Ngaramtoni kuwa ni ya mkoa ili apate fedha kutoka Serikali kuu na ijengwe kwa kiwango cha Lami.
#Amewahoji wananchi waliojenga pembezoni mwa barabara hiyo endapo wako tayari, kusogeza nyumba zao ili ufanyike upanuzi wa barabara na kuweza kujengwa kwa kiwango cha Lami, bila kumung'unya maneno wananchi hao waliitikia ndiyo kwa kushangilia,
#Amewataka viongozi waliochaguliwa na wananchi , ikiwemo Wabunge na Madiwani kuwatumikia wananchi waliowachagua ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitatua.
#Kuendelea kutatua changamoto ya Umeme, na endapo Mkandarasi kama ameshindwa kufanya kazi yake aondolewe.
# Viongozi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanajenga mnada wa kuuzia Ng'ombe katika maeneo ya mipaka ili wananchi wapate fursa yakupata masoko ya nje.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Olmringaringa kata ya Kimnyaki.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Olmringaringa kata ya Kimnyaki.
Baadhi ya wananchi wilayani Arumeru wakifuatilia hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Olmringaringa kata ya Kimnyaki.
Baadhi ya wananchi wilayani Arumeru wakimsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Olmringaringa kata ya Kimnyaki.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.