• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC: Elimu ya malezi na makuzi ya mtoto kuanza kutolewa kliniki ya mama na mtoto

Posted on: April 22nd, 2018

 Watu wengi wamekua na tabia ambazo ni kinyume na maadili, tabia ambazo hata mzazi anashangaa mtoto wake amezipata wapi, lakini kwa asilimia 80, tabia ya mtoto inajengwa na mzazi na mlezi kuanzia mimba mpaka umri wa miaka mitatu.

Kutokana na uelewa mdogo wa wazazi na kushindwa kupembua mambo chanya ya kumjengea mtoto katika umri huo,husababisha mtoto kushindwa kujitawala na kutawala mazingira yanayomzunguka kiakili, kimwili, kihisia na kisaikolojia.

Tafiti zinaonyesha kuwa elimu duni ya wazazi na walezi juu ya malezi na makuzi ya mtoto husababisha udumavu kwa watoto kimwili, kiakili na kisaikolojia.

Tabia anazokuwa nazo mtu mzima, ziwe mbaya au nzuri ni matokeo yaliyojengeka kwa mtoto kuanzia kipindi cha mimba mpaka alipofikisha umri wa miaka mitatu.

Ubongo wa mtoto, unategemea zaidi kupewa/ kujazwa vitu kutoka kwa wazazi na walezi pamoja na watu wanaomzunguka kuanzia kipindi cha mimba mpaka miaka mitatu ili uweze kukua na kumjenga mtoto huyu uwezo wa utambuzi.

Hayo yamethibitishwa na Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi, wakati akitoa mafunzo kwa wauguzi wa afya wa kitengo cha huduma za mama na mtoto wa halmashauri ya Arusha na Jiji la Arusha,  yaliyofanyika kwenye ukumbi wa SEDHA Jijini Arusha.

Afisa Ustawi huyo na mwezeshaji wa mafunzo hayo amesema kuwa, wauguzi waliopata mafunzo hayo, wanakwenda kutoa mafunzo juu ya vichocheo changamshi muhimu kwenye makuzi ya mtoto kwa wazazi na walezi kila wanapofika Kliniki kuanzia wakati wa kliniki ya mama mjauzito na mara baada ya mtoto kuzaliwa mpaka miaka mitano.

Aidha Afisa Usatawi huyo amesema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuelewa umuhimu wa kufahamu  mambo yakuzingatia katika hatua za malezi na makuzi ya mtoto, kuanzia mimba mpaka miaka mitatu ndio yanayojenga mtoto kuwa na tabia nzuri au mbaya.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha mimba mpaka miaka mitatu,mtoto anatakiwa kupewa elimu changamshi yenye vichocheo chanya, itakayoanza kumjengea uwezo mtoto wa kukua kimwili, kiakili na kisaikolojia.

Kwa mtoto  mpaka kufikia umri wa miaka mitatu, ubongo wa mtoto unakuwa tayari umejaa kwa asilimia 80, asilima 20 iliyobaki, huongezeka kwa kipindi kilichosalia cha maisha yake yote.  

Hivyo katika umri huu ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha wanamjenga na kumjaza mtoto maadili  mema yatatayomfanya mtoto kuwa na mitazamo chanya itakayomuwezesha kufanikiwa katika maisha yake ya baadae.

Vichocheo chanya kutoka kwa wazazi na walezi na vinamfanya mtoto aweze kujitambua, kujiamini, kujifunza zaidi na uwezo wa kupembua mema na mabaya, hivyo wazazi na walezi wana jukumu kubwa sana la malezi ya mtoto mpaka atakapofikisha umri wa miaka mitatu" amesema Tengi.

Endapo mtoto atakosa vichocheo chanya ni dhahiri mtoto huyu atakua hajiamini, uwezo mdogo wa kujifunza, hawezi kujitegemea, muoga na mwenye wasiwasi na kuwa na mahusiano mabaya na jamii katika maisha yake.  

 Tengi ameongeza kuwa kipindi chote cha ujauzito mtoto anatakiwa kujazwa mambo mema ikiwemo upenda na kujaliwa na baada ya kuzaliwa mpaka miaka mitatu mtoto anapaswa kufundishwa mambo chanya ya kijamii.

Hata hivyo Tengi amethibitisha kuwa makosa yanayofanywa na wazazi na walezi kwenye hatua za  malezi na makuzi ya mtoto yanamadhara makubwa sana kwa maisha ya mtoto hasa anapokuwa mtu mzima.

Amewataka wazazi na walezi kushirikiana katika hatua zote za makuzi ya mtoto kwa kumchochea vichangamshi chanya na kuongeza kuwa wazazi ni lazima kuzungumza na mtoto mambo mema, kuacha kutukana, kumsemea mtoto mambaya badala yake kumuonyesha upendo zaidi, kumjali na kumfanya ajitambue,ajiamini, ajithamini na kuthamini wengine kuanzia anapozaliwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.