Na .Elinipa Lupembe.
Timu ya watalamu wa Benki ya NMB Arusha, wamemtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha, na kufanya mazungumzo ya kina juu ya ushirikiano wa Benki hiyo na halmashuri ya Arusha, ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya serikali ya awamu ya tano ya kusogez huduma wananchi katika maeneneo yao ili kuharakisha maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Watalamu hao wakiongozwa na Meneja wa Banki ya NMB tawi la Clock Tower la Jijini Arusha, Emmanuel Kishosha, amesema kuwa NMB benk, imepanga kudumisha ushirikiano na halmashauri hiyo, hasa katika masuala ya kibenki pamoja na masuala mengine ya kijamii yahusuyo mambo ya kifedha.
Hata hivyo watalamu hao wa NMB walimkabidhi zawadi za Kalenda na 'note book' kwa mkurungenzi mtendaji wa halamshauri hiyo, ikiwa ni ishara ya kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Benki hiyo na halmashauri katika kuwahudumia wananchi wa hali zote.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, licha ya kuwashukuru watalamu wa Benki hiyo ya NMB, ameahidi kuendelea kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Benki hiyo, benki inayowahudumia wananchi wa halmashauri hiyo hasa kwa kusogeza huduma karibu na wananchi mpaka katika maeneo ya pembezoni kwa gharama ambazo wananchi wanazimudu.
"Ninaishukuru benki ya NMB, licha ya kwamba sisi ni wateja wenu, lakini pia mmekuwa wadau wetu wa kubwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika halmashauri yetu, kila tunapowahitaji mmekuwa wepesi kujitokeza, mmekuwa mkitoa huduma za kibenki kwa wanachi wetu hadi latika maeneo ya pembezoni, jambo ambalo linaharakisha upatikanaji wa huduma na kuchochea maendeleo ya kiuchumimna kijamii' amethibitisha Mkurugenzi Mtambule
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.