Na. Elinipa Lupembe.
Hayawi hayawi yamekuwa, hatimaye leo viongozi wa halmashauri mbili za Arusha na Meru zinazounda wilaya ya Arumeru, wamekubaliana kwa pamoja kugawana eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 3,380, lililoko eneo la Engira Road Jijini Arusha.
Awali eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na iliyokuwa halmashauri ya Arumeru, ambayo ilivunjwa na 30Juni 2007 na tarehe 01 Julai, 2007 kuzaliwa halmashauri mbili za Arusha na Meru na kulazimika kugawana baadhi ya mali zilizokuwa zikimilikiwa na halmashauri hiyo ya Arumeru.
Makubaliano hayo yamefikiwa mara baada ya pande zote mbili, kukaa vikao vya kisheria katika halmashauri husika na hatimaye kukutana kwenye kikao cha pamoja, kilichosimamiwa na kuongozwa na Katibu Tawala wilaya ya Aruemru, Mwalimu James Mchembe, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru.
Katika kikao hicho kilichojumuisha Waheshimiwa Madiwani wa Kamati ya Fedha Utawana na Mipango na timu ya Menejimenti ya halmashuri zote mbili za Arusha na Meru, na kufikia makubaliano ya kugawana eneo hilo nusu kwa nusu bila kujali majengo yaliyopo katika eneo hilo.
Aidha mgawanyo wa eneo hilo lenye Mita za mraba 3,389 utawezesha halmashauri ya Arusha kupata Mita za mraba ,1,690 kadhalika halmashauri ya Meru kupata mita za mraba1,690 pia.
Hata hivyo, baada ya makubaliano hayo, viongozi hao wamewaagiza watalamu wa Ardhi wa pande zote mbili kuanza mchakato wa kugawa eneo hilo kwa haraka na kupata hati miliki ya kila eneo, ili kila halmashauri iwe na hati miliki yake pamoja na kuanza kutumia maeneo hayo kwa manufaa ya wanachi wa halmashauri zote mbili.
ARUMERU
KaziInaendelea✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.