• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC: Wauguzi watakiwa kuacha tabia ya kufanya kazi ya Uuguzi kama biashara

Posted on: February 22nd, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Wauguzi halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuacha tabia ya kufanya kazi ya uuguzi kama biashara, na badala yake kufanyakazi hiyo kwa weledi, kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ya uuguzi, huku wakiongozwa na imani, heshima, upendo, upole, unyenyekevu na uvumilivu.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Utumishi, halmashauri ya Arusha,  Juma Mpume wakati akifungua kikao kazi,  kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, kilichowakutanisha wauguzi wanaotoa huduma kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya serikali na binafsi ndani ya halmashauri ya Arusha, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mpume amefafanua kuwa, taaluma ya uuguzi ni taaluma nyeti, ambayo inagusa uhai wa binadamu, hivyo inahitaji unyenyekevu, upendo na kuwataka wauguzi hao kuwa na imani pindi wanapowahudumia wagonjwa, na kujikita kutoa huduma kwa weledi na kufuata miongozo inayoongoza taaluma ya uuguzi kwa wagonjwa.

Amefafanua kuwa, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na wauguzi, bado kuna malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa, juu ya rushwa na lugha chafu, iwe hospitali za Serikali hata zile za binafsi, tabia ambayo ni kinyume cha maadili ya utumishi wa Umma na maadili ya Uuguzi pia.

Aidha Mpume, amewaonya baadhi ya wauguzi wasio waaminifu, wanaochafua taaluma hiyo, kwa kudai rushwa na kutoa lugha mbaya  kwa wagonjwa, kuacha mara moja tabia hiyo, tabia ambayo licha ya kuwaathiri wagonjwa kisaikolojia, inachafua weledi wa taaluma ya Uuguzi kwa ujumla wake.

"Kazi yenu inagusa maisha ya binadamu, haihitaji mzaha wala vipingamizi, wahurumieni wagonjwa, kuweni makini kuokoa maisha yao, wale wanaotaka chochote kabla ya kutoa huduma waache tabia hiyo, tambueni kufanya hivyo kuna madhara makubwa kwa  wagonjwa na jamii kwa ujumla wake " Amesema Mpume.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Dkt. Wedson Sichalwe, alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na wauguzi hao, kutokana na kuhamia kufanyakazi kwenye mkoa wa Arusha, na kuanza kwa kuwapongeza wauguzi hao,  kwa kufanya kazi kwa bidii licha ya changamoto ndogo zinatokana na baadhi ya wauguzi wasio waaminifu.

Mganga mkuu huyo, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imetoa kipaumbele kikubwa kwenye Sekta ya Afya, kwa kuboresha miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa lengo la kuhakikisha, watoa huduma za afya wanafanya kazi kwenye mazingira rafiki yatakayowezesha, mwananchi kupata huduma bora kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya hadi hospitali.

Ili kufikia lengo la Serikali la kuboresha  upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi  na kupunguza vifo vya mama na mtoto, Wauguzi ndio kiungo cha kufikia malengo hayo, kwa kuhakikisha kila mtu anayefika kwenye kituo cha afya anapata huduma bora na stahiki.

Aidha Dkt. Sichalwe, amewashauri kuweka kipaumbele katika upatikanaji wa maji na umeme, kwenye vituo vyao vya afya kupitia bajeti zao za vituoni, huduma ambayo ni muhimu sana kwenye vituo vya afya.

Hata hivyo wauguzi hao, wamekiri bado kuwepo na wauguzi wachache, wanaoichafua taaluma hiyo kwa kudai rushwa na kutumia lugha ambayo si rafiki kwa wagonjwa, na kuahidi kuendelea kurekebishana na kuonyana kama binadamu, huku wakiahidi kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi mkoa wa Arusha (TANNA) na muuguzi, Sista Gladness Mtui ameshukuru  uwepo wa kikao kazi hicho ambacho kimetumika kuwanoa upya na kuwakumbusha wauguzi maadili ya kazi zao, na kuahidi kuendelea kusimamia maadili ya taaluma yao, nyeti  ya uuguzi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.