Halmashauri ya Arusha imeadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike, kwa wasichana wanafunzi vinara wa kupinga ukatili nyumbani na shuleni kutoka shule 8 za halmashauri hiuo kufanya maandamani na midahalo na maonesho ya kazi za mikono.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye shule ya sekondari Einoth kata ya Kisongo, yenye Kauli mbiu ya “Haki Zetu ni Hatima Yetu; Wakati ni Sasa" huku wasichana hao wakiwa na malengo ya kupinga ukatili nyumbani na shuleni.
Katika maadhimisho hayo, wasichana vinara wamehimiza utoaji wa haki sawa kwa Watoto wote bila ubaguzi wowote.
Hata hivyo katika miaka 10 ya utekelezaji wa haki za watoto, umakini umeongezeka katika kuainisha na kusimamia upatikanaji wa haki kwa watoto wote huku mkazo zaidi ukiwekwa kwa watoto wa kike.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwa ushirkiano wa halmashauri ya Arusha na shirika la HakiElimu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.