• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC yaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kipekee

Posted on: June 20th, 2018

Katika kuendelea kukabiliana na vitendo na matukio ya ukatili dhidi ya watoto, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, imefanya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa njia ya pekee kwa kuwashirikisha watoto waliokumbana na changamoto ya matukio ya ukatili ikiwemo kukeketwa, kuchumbiwa wangali shuleni na wengine kuozeshwa.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya chuo cha ufundi stadi Mwandeti kata ya Mwandeti huku watoto hao wakitoa kilio chao kwa serikalo juu ya kuimarisha ulinzi juu yao, kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

Watoto hao wamewataka wazazi kutambua na kuthamini haki zao na zaidi kuimarisha miundo mbinu ya ulinzi dhidi ya ukatili unafanyika ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

Akizingumza wakati wa sherehe hizo, mgeni rasmi na mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera amesema kuwa halmashauri imejipanga kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya ukatili na kuwataka wazazi na jamii nzima kushiriki kuwalinda watoto.

Ameongeza kuwa licha ya mila na desturi potofu za jamii ya wenyeji wa maeneo hayo zinafanya kwa siri ukeketaji lakini mkurugenzi huyo ameitaka jamii kuacha mara moja tabia hiyo na kuwataka watoto kutoa taarifa pale wanapofanyiwa au kutaka kufanyiwa ukatili wa aina wowote.

Hata hivyo, mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yanayofanyakazi katika halmashauri hiyo, wametangaza kushirikiana  na Serikali katika kupata muarobaini wa matukio ya ukatili yanayowakabili watoto, ndani ya  halmashauri hiyo.  

Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya Ace Africa na WDCD wamejikita kwenye uwezeshaji watoto katika shule kwa kuanzisha klabu shuleni ambazo zinawawezesha watoto kutambua haki na wajibu wao, pamoja na kutoa taarifa pale wanapofanyiwa ukatili.

Aidha wadau hao, wamewataka watoto kutumia mbinu na stadi za maisha wanazopewa, kwa kuwa mbinu hizo zitawawezesha watoto hao kujitambua, kujisimamia pamoja na kukua katika maadili, yanayowawezesha kujitegemea na kujiajiri katika sekata ya kilimo na viwanda.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.