Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha katiika kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi, na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma stahiki na kwa wakati, Halmashauri imewataeua watalamu wa sekta za Kilimo, Mifugo, Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya kata, kufanyakazi kwenye vitongoji hivyo, kwa kusaidiana na Afisa Mtendaji wa Kata kwenye kata saba za Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.
Mpango mkakati huo umekuja mara baada ya vilivyokuwa vijiji katika kata hizo saba kupandishwa hadhi na kuwa vitingoji kwa mujibu wa kanuni na kuondolewa waliokuwa Maafisa Watendaji wa Vijiji katika Mamlaka hiyo ya Mji Mdogo Ngaramtoni.Akijibu Maswali ya Papo kwa papo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, swali lililouzwa na Diwani wa kata ya Kiranyi, mheshimiwa John Seneu, aliyetaka ufafanuzi upi mkakati wa halmashauri wa kuhakikisha wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni wanapata huduma kutoka kwa wataalamu kutokana na ukweli kwamba kata hizo saba zinasimamiwa na Afisa Mtendaji wa kata tu, huku kukiwa na idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji huduma katika ofisi ya kata.
Mkurugenzi Mtambule, amefafanua kuwa, tayari halmashauri imewapangia watalamu wa sekta zote walioko kwenye ngazi ya kata, pamoja na majukumu yao, kusaidia kusimamia shughuli nyingine katika maeeneo ya kata hizo,lengo likiwa ni kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa wananchi wa maeneo yote ya Mamlaka ya Mji Mdogo."Ili kuhakikisha wananchi wa kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni, tumewaongezea na kuwapangia majukumu, watalamu wa kilimo, mifugo,Elimu na Maendeleo ya Jamii, kufanyakazi katika maeneo hayo, ili kuharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi, wakati tukisubiri kibali cha kuajiri kutoka serikali kuu" amesema Mkurugenzi Mtambule.
Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni, ilianzishwa rasmi Oktoba 2014 kwa mujibu wa sheria ikiwa na kata saba za Moivo, Ilboru, Kiranyi, Tarakwa, Oloirien, Olmotony na Olturumet.
Mkurugenzi Saad Mtambule, akijibu maswali ya papo kwa papo, wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2020/2021,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani, wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2020/2021,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.