Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru imepata Hati Safi kwenye ukaguzi wa hesabu kwa mwaka wa nne mfululizo sasa.
Hati hiyo safi imepatikana kufuatia taarifa iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad, aliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii ofisini kwake Jijini Dodoma.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amesema kuwa amafurahishwa sana na halmashauri yake, kupata hati safi kwa mara ya nne mfululizo na kuongeza kuwa hati hiyo imetokana na utendaji mzuri na ushirikiano wa watumishi walio chini yake.
Aidha mkurugenzi huyo, amewapongeza watumishi wote wa halmashauri ya Arusha kwa ujumla wao, wakuu wa idara na vitengo pamoja na Baraza la Waheshimiwa Madiwani, kwa pamoja ndio waliofanikisha upatikanaji wa hayo hiyo safi.
Mweka Hazina wa Halmshauri ya Arusha, Ritte Wiliam amesema siri ya kupata hati safi ni matumizi ya fedha yanayozingatia sheria, kanuni na taratibu ya fedha za umma pamoja na watumishi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Ritte amesema kuwa, halmashauri inamkakati wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha halmashauri hiyo inaendelea kupata hati safi.
Mwandishi anatoa hongera sna, kwa watumishi wote ARUSHA DC, na kuwataka wachape kazi kwa weledi kwa kuweka mbele uzalendo.
#PamojaTunatekeleza#PAMOJATUNATEKELEZA#
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.