• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC yapokea pikipiki 18 kwa ajili ya Maafisa Elimu Kata

Posted on: August 15th, 2018

Halmashauri ya wilaya wa Arusha imepokea jumla ya pikipiki 18 kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za elimu kwa ngazi ya kata, pikipiki ambazo zitatumiwa na Maafisa Elimu ngazi ya kata, kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za elimu kwenye shule wanazozisimamia ndani ya kata zao.

Akizungumza mara baada ya kupokea pikipiki hizo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera amesema kuwa, pikipiki hizo zitakuwa chachu ya uwajibikaji hasa katika kurahisisha utendaji kazi kwa maafisa elimu wa ngazi ya kata.

Ameongeza kuwa kulingana ya Jiografia ya halmashauri ya Arusha, hasa kwa kata za pembezoni, kuna umbali mkubwa kutoka shule moja na nyingine, jambo lililokuwa linawawia vigumu  maafisa elimu hao, kuratibu shughuli zao kwa ufanisi.

Hata hivyo amethibitisha kuwa, kutokana na uwepo wa vitendea kazi hivyo, anaamini sekta ya elimu kuendelea kuboreka zaidi kwa kuwa na usimamizi mzuri katika ukusanyaji wa taarifa pamoja na ukaguzi wa utendaji kazi wa walimu na shule kwa ujumla.

" Kwa kuwa sasa maafisa elimu wamepata usafiri, naamini watakwenda kusimamia vizuri utendaji kazi wa walimu shule, ukusanyaji wa takwimu na usimamizi wa shule kwa ujumla wake huku tukitegemea kupandisha taaluma pamoja na kuongeza ufaulu" amesema Mkurugenzi Mahera.

Naye Kaimu Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, Charles John amesema kuwa,, pikipiki hizo zitakwenda kutatua changamoto nyingi shuleni, kutokana na ugumu uliokuwepo kwa baadhi ya maeneo, wa kuzifikia shule kwa wakati.

"Kulikuwa na ugumu kwa Afisa Elimu kata kutembelea kwa mguu kukagua shughuli za utendaji shuleni kutoka na umbali mrefu wa kutoka shule moja mpaka nyingine, lakini kupatikana kwa usafiri huu kutarahisha kuzifikia shule na kuwa na usimamizi thabiti" amesema Afisa Elimu huyo.

Januari  Ambros, mkazi wa Sakina ameipongeza serikali ya awamu ya tano, kwa kuona umuhimu wa kutoa vitendea kazi kwa ajili ya kurahisisha usimamizi na ukaguzi wa kazi zinazofanywa ma walimu na wanafunzi shuleni.

Licha ya pongezi hizo Ambros,  ameiomba serikali, kuangalia namna ya kuwapanga wanafunzi  wanaokwenda sekondari kwenye shule za jirani au kujenga mabweni ili kuondoa changamoto kubwa wanayoipata watoto njiani wakati wa kwenda na kurudi nyumbani.

"Watoto wanajikuta wamejiingiza kwenye vitendo vibaya ikiwemo mimba na uvutaji wa bangi, wanapokutana na watu wasio wema njiani na kujikuta wanashawishika kuingia kwenye mitego ambayo mwisho huwa na madhara makubwa kwa wanafunzi hao" amesema Ambrosi.

Serikali ya awamu ya tano, inaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutatua changamoto za elimu ikiwemo kutoa elimu bila malipo, miradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule kupitia miradi ya P4R pamoja na kuanza kutoa vyombo vya usafiri kwa Maafisa Elimu kata kwenye halmashauri nchini.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.