Na. Elinipa Lupembe
Halmashauri ya Arusha imepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 16.6 , kutoka kwenye Asas ya kiraia ya Kilmanjaro Technology Foundation, kwa ajili ya kujinga na kupambana na ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virus vya Covid 19.
Akikabidhi vifaa hivyo, kwenye ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa Kilimanjaro Technology Foundation, Lidya Maliti, amesema kuwa, shirika limeamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kupambana na gonjwa la hatari la Corona kwa kutoa vifaa hivyo, vitumike kwenye taasisi za Umma, kwa lengo la kujikinga na gonjwa hilo.
"Ugonjwa wa Corona upo, inatubidi tuishi nao kwa kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni katika maeneo yetu ya kazi, huku tukiendelea kuchapa kazi na kulijenga taifa letu, kama mheshimiwa Rais wetu alivyoelekeza" amesema Meneja huyo
Imeelezwa kuwa vifaa vilivyotolewa vina thamani ya shilingi milioni 16.6, ikiwa ni pamoja na Ndoo 1000 za kunawia mikono, Barakoa 1000 za vitambaa kwa ajili ya watumishi wa Umma na Barakoa nyingine 1,000 'surgical mask' kwa ajili ya wahudumu wa afya.
Meneja Lidya ameelekeza vifaa hivyo kugawiwa kwenye ofisi za taasisi za Umma, ndani ya halmashauri hiyo, ikiwemo ofisi za makao makuu, ofisi za kata na vijiji, masoko na minada, vituo vya afya na zahanati zote, shule za msingi na sekondari, Mahakama, kituo cha Polisi vilivyopo kwenye halmashauri ya Arusha.
Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha, Paulus Kessy, mbali na kuishukuru ASAS hiyo kwa msaada huo, ameeleza kuwa, vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka ambapo, wananchi wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao za kila siku huku wakitakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya gonjwa hatari la Corona, kwa kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa pamoja na kutumia vitasa mikono.
Aidha Kaimu mkurugenzi huyo, amewataka wananchi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kufanyakazi kwa bidii, sambamba na kuchukua tahadhali kwa kujikinga na gonjwa la Corona, zaidi kufuata maelekezo ya Serikali na yanayotolewa na watalamu wa Afya.
Msimamizi wa Ofisi, halmashauri ya Arusha, Grace Mburuja, amesema kuwa, vifaa hivyo ni muhimu kwa watumishi wa taasisi za serikali kwani wao, huwahudumia wananchi wengi kutoka maeneo tofauti, kupitia vifaa hivyo watumishi watafanyakazi kwa uhuru bila hofu ya kupata maambukizi ya Corona.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawahimiza wananchi wote, kuendelea kuchukua tahadhari ya gonjwa la Coron kwa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono 'sanitizer' na kuvaa Barakoa wakati wote wakiwa kazini hasa kwenye mikusanyiko.
Kaimu mkurugenzi halmashauri ya Arusha, Paulus Kessy akipokea ndoo ya kunawia mikono kutoka kwa Meneja wa Asas ya kiraia ya Kilimanjaro Technology Foundation Lidya Maliti.
Kaimu mkurugenzi halmashauri ya Arusha, Paulus Kessy akipokea barakoa tiba 'surgical mask' kwa ajili ya wahudumu wa afya wa halmashauri hiyo, kutoka kwa Meneja wa Asas ya kiraia ya Kilimanjaro Technology Foundation Lidya Maliti, kulia ni Afisa Elimu Msing, mwalimu Hossein Mghewa.
Kaimu mkurugenzi halmashauri ya Arusha, Paulus Kessy akipokea barakoa za kitambaa kwa ajili ya watumishi wa Umma wa halmashauri hiyo, kutoka kwa Meneja wa Asas ya kiraia ya Kilimanjaro Technology Foundation Lidya Maliti.
Mganga Mkuu, halmashauri ya Arusha, Dkt. Petro Mbaya,akiwa na barakoa tiba 'surgical mask' kwa ajili ya wahudumu wa afya wa halmashauri hiyo, tayari kwa kwenda kuanza kuanza kazi ya kuwahudumia wagonjwa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.