Na. Elinipa Lupmebe.
Halmashauri ya Arusha, imeanza rasmi kutekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa na serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwa halmasahuri zote nchini kutumia mapato ya ndani kujenga kituo cha afya.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amesema kuwa, halmashauri yake, imeanza rasmi ujenzi wa kituo kipya cha afya cha Mateves, katika kata ya Matevesi, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, maagizo yaliyoelekeza kila halmasahuri kutumia shilingi milioni 500, fedha za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kujenga kituo cha afya kwa kata ambazo hazina vituo vya afya.
Mkurugenzi Msumi, ameweka wazi kuwa, halmashauri imeanza kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya Mateves, kwa kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), mradi utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 310 kwa awamu ya kwanza.
"Kata ya Mateves ni mingoni mwa kata zenye idadi kubwa ya watu lakini hikuwa na kituo cha afya cha serikali, tumeona ni vyema kuelekeza nguvu za ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo, ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi wa maeneo hayo, na kutimiza lengo la serikali la kuwa na kituo cha afya kwa kila kata" amesema Mkurugenzi Msumi.
Naye Afisa Mipango Mkuu, halmashauri ya Arusha, Anna Urio, amefafanua kuwa, mpaka kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa kituo cha afya Mateves, utagharimu kiasi cha shilingi milioni 500, ambapo kwa wamu ya kwanza umeanza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022, halmashauri ya Arusha imefanikisha ujenzi wa vituo vitatu vya afya, ikiwemo kituo kipya cha Afya cha Mwandet, kinachojenhwa kwa fedha kutoka serikali kuu, huku vituo viwili vikijengwa kwa mapato ya ndani, kituo kipya cha afya cha Oloirieni na kituo kipya Mateves vyote vikijengwa kwa fedha za mapato ya ndani.
.ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi ( mwenye kofia), akichimba msingi wa ujenzi wa kituo kipya cha afya cha Mateves, mradi ulioanza kutekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.